MASIGNCLEAN101

Aina za Viambishi

Aina za Viambishi
citylab
Monday, 1 February 2021
 

 Aina za Viambishi

Ziko aina kuu tatu za viambishi vinavyonatishwa kwenye mzizi, nazo ni:
(i) Viambishi awali
Kati ya hivi Viambishi vya mwanzoni mwanzoni mwa mzizi, kuna:
(a) kile cha kwanza kabisa ambacho kiko mbali na mzizi ambacho hujulikana ama Kiambishi
Ngeli, au
Kiambishi cha Idadi, au Kiambishi Nafsi (mtenda, mtendwa au mtendewa).
(b) kile cha kwanza kabisa kinachogusana na mzizi.
(c) kile kilichoko/vile vilivyoko kati ya kile cha kwanza kabisa ambacho kiko mbali na mzizi na
kile cha kwanzakabisa kinachogusana na mzizi.
Kwa mfano, katika neno tutampiganisha (= tu-ta-m -pig - an-ish-a) :
tu-ta-m- ni viambishi vya mwanzoni mwanzoni mwa mzizi, -pig-.
tu- ni kiambishi cha kwanza kabisa ambacho kiko mbali na mzizi, -pig-, (mtenda).
-m- ni kiambishi cha kwanza kabisa kinachogusana na mzizi, -pig-, (mtendwa).
(d) -ta- ni kiambishi kilichoko kati ya kile cha kwanza kabisa ambacho kiko mbali na mzizi na kile
cha kwanza kabisa kinachogusana na mzizi, -pig, (njeo ijayo). 104
(ii) Viambishi Tamati
Kati ya hivi Viambishi tamatii, kuna:
(a) kile cha mwisho kabisa ambacho kiko mbali na mzizi na ambacho aghalabu huitwa
kiambishi tamatishi.
(b) kile cha mwisho, lakini cha kwanza kugusana na mzizi.
(c) kile kilichoko/vilivyoko kati ya kile cha mwisho kabisa ambacho kiko mbali na mzizi
na kile cha mwisho, lakini cha kwanza kugusana na mzizi.
Kwa mfano, katika neno tutampiganisha (tu-ta-m -pig - an-ish-a)
-an-ish-a ni viambishi vya mwishoni mwishoni mwa mzizi, -pig-.
-a ni kiambishi cha mwisho kabisa ambacho kiko mbali na mzizi, -pig-, (kiyakinishi
cha kauli).
-an- ni kiambishi cha kwanza kabisa kinachogusana na mzizi, -pig-, (kitendeana cha
kauli).
-ish- ni kiambishi kilichoko kati ya kile cha mwisho kabisa [a} ambacho kiko mbali
na mzizi na kile cha kwanza kabisa {an} kinachogusana na mzizi, -pig-, (kitendea cha
kauli).
 Dhima ya Viambishi Katika Neno
Viambishi vya mnyambuliko vyote hubadili sana hali na tabia ya neno, kama ifuatavyo:
(a) Jinsi kitenzikinavyozidi kupokea viambishi vya mnyambuliko, ndivyo kitenzikinavyozidi
kujijengea mizizi na mashina mapya
   
Kwa mfano:
Kitenzi Mzizi Shina Mnyambulisho Mzizi wa Shina Mnyambulisho
piga pig- piga pigana pigan- pigana105
Aidha, kitenzi hicho hicho kinaweza kujengeka upya na kupata hali na tabia za kipashio
kipya, kama vile nomino:
Kitenzi Nomino
pig-a (i) pig-o,
(ii) ma-pig-o,
(iii) pig-an-o,
(iv) ma-pig-an-o.

b) Viambishi vya mnyambuliko huyafanya maneno yabadili asili yake ya kipashio na kuwa
kipashio kipya na kupokea tabia na hali zote za kipashio hicho kipya, kwa mfano:
(i) mtulivu (N) => tuli-a (T) => tulizan-a (T) => tulivu (V) =>
mtulizaji (N) =>tuli (E).
(ii) msafishaji (N) =>safisha (T)=>safishan-a (T) =>
safi (V).
(iii) mkaribishaji (N) => karibi-a (T) => karibish-a (T) => karibishan-a
( T) => karibish-o (J )
(iv) sawa (V) => sawazish-a (T) => sawazish-o(N).


(c) Baadhi ya vivumishi hupokea kiambishi awali ki- au vi- na kuweza kufanya kazi ya kielezi, kwa
mfano:
(i) zuri (V) => vi-zuri;
(ii) ema (V) => vy-ema, v-ema;
(iii) kubwa => ki-kubwa.


Share This :
...