MASIGNCLEAN101

Aina za Maana

Aina za Maana
citylab
Monday 1 February 2021

 

Aina za Maana
Wanaisimu mbalimbali wameeleza dhana ya aina za maana katika vitengo viwili vikuu; maana ya
msingi na maana ya ziada. Hata hivyo Leech (1981) amebainisha aina za maana zifuatazo:
 1 Maana ya msingi (conceptual meaning)
- Hii ni aina ya maana ambayo haibadiliki mfano; mwanamke, mwanaume. Hutaja sifa zake kuu. Zile
sifa bainifu ndizo hupelekea kupata maana kuhusu mtu.

2 Maana dokezi (connotative meaning)
- Ni aina ya maana ambayo hutokana na umbo la kitu, kisaikolojia, kimatamshi mf. Kiumbo kushika
mimba, kisaikolojia umama.

3 Maana ya kijamii / kimtindo (social meaning)
- Ni aina ya maana ambayo hupatikana kutokana na mazingira ya kijamii, wakati, utamaduni,
kijiografia, kiuwasilishaji, hadhi, ubinafsi n.k

4 Maana ya kihisi (emotive meaning)
- Ni maana za kihisia ambazo hutokana na upotoshaji wa aina fulani wa maana ya msingi. Ni maana
itokanayo na utumizi usio wa moja kwa moja ili kutoa maana. Maana ya kitu huwa ni ya mzunguko,
fiche, kwa mfano maana za hisia hutegemea sana Kiimbo kiwekwacho katika neno au Kiimbo
kiwekwacho katika sentensi.

5 Maana tangamani (collocative meaning)
- Maana ambatani au tangamano, ni aina ya maana itokanayo na utangamano au uambatani wa
baadhi ya maneno kwa mfano: Mrembo – Msichana
: Ujamali – Mvulana
150: Jitu hili ni la miraba mine – Mwanaume
- Katika lugha maneno pia hujengwa kwa mtindo huo mifano zaidi Samaki – Kiumbe wa
majini/baharini au Swala - Kiumbe wa msituni. Ukitaja kimoja tu mfano samaki unakuwa
umekiondoa kingine swala.

6 Maana ya kidhima/kidhamira (thematic meaning)
- Hizi ni aiana za maana ambazo ujumbe wake unapangwa kufuatana na msisitizo wa kitu. Maana
hutokana na dhamira ambayo msemaji alikusudia ili imfikie msikilizaji, kwa mfano sentensi zifuatazo:
- (a) Mwalimu amempiga mtoto (Mwl. Mtenda)
- (b) Mtoto amepigwa na mwalimu (Mtoto Mtendwa)
- (c) Msichana yupo darasani (Jibu la swali lililoulizwa) – Msichana yuko wapi?
- (d) Darasani kuna msichana (Swali)

7 Maana akisi/Kimwangwi (reflected meaning)
- Ni maana ambazo ukitaji kitu fulani au maana fulani unakonyeza maana nyingine. Maana akisi
haziachani kwa mfano: Jamii – Mkusanyiko wa watu pamoja

Uhusiano wa Maana
Katika taaluma ya semantiki, kuna uhusiano wa aina tatu wa maana; Utajo, Urejeleo na Fahiwati.

1 Utajo (Notion).
Huu ni uhusiano wa maana kutokana na kutaja kitu kama kilivyo katika ulimwengu halisi. Utajo
hutaja kitu kama kilivyo kwa ujumla. Kwa mfano dhana ya meza katika ulimwengu huu
tunaoufahamu maana zake ni nyingi lakini kuna sifa za kisemantiki zinazotofautisha meza na kitu
kingine katika utamaduni. Kamusi moja (D. Crystal (1991: 97)* ilifafanua kuwa maana ya utajo ni
sawa sawa na maana ya Kiurejeleo. Katika kubainisha maana kiutajo, rejelea sifa za kisemantiki
unazozifahamu kimalimwengu. Mfano Mwanaume au Mwanamke (taja sifa za kila mmoja).
Utajo huhusu uhusiano baina ya leksimu au kipashio cha kiisimu na seti ya vitu ambayo inarejelewa
na kipashio hicho katika ulimwengu halisi. Kwa mfano, utajo wa leksimu meza ni vitu vyote katika
Share This :
...