MASIGNCLEAN101

MCHANGO WA TAFSIRI KATIKA UKUAJI WATAMTHILIA YA KISWAHILI

MCHANGO WA TAFSIRI KATIKA UKUAJI WATAMTHILIA YA KISWAHILI
citylab
Sunday 29 May 2022
SWAHILI LAB
MCHANGO WA TAFSIRI KATIKA UKUAJI WATAMTHILIA YA KISWAHILI..
LEARN SWAHILI 11:45:00  1


UTANGULIZI:
Dhana ya tafsiri na tamthiliya kuswahili:
Catford (1965:20) anasema tafsiri ni kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha moja (lugha chanzi) na kuweka badala yake mawazo yaliyolingana katika lugha nyingine (lugha lengwa).
Mwansoko, (2006) anafasili neno tafsiri ni zoezi la kuhawilisha ujumbe kutoka matini chanzi kwenda matini lengwa.

Kwa mujibu wa Wafula, (1999).Anaeleza kuwa kuna aina nne za tamthiliya zilizo tafsiriwa kama ifuatavyo, kwanza kuna tamthiliya zilizo tafsiriwa kutoka lugha nyingine hadi kiingereza na kisha kutafsiriwa kwa Kiswahili,mfano wa tamthiiya hizo ni pamoja na “mchuuzi muungwana”yake Moliere, nyingine ni “Mfalme Edipode” yake Mbunda Msokile na ile ya “Mkaguzi Mkuu wa Serikali” yake Nikolai Gogol.

Pia kuna zile tamthilia zilizo andikwa kwa kiingereza na wageni na kutafsiriwa kwa Kiswahili mfano wa tamthilia ilizo tafsiriwa katika mfumo huu ni pamoja na tamthiliya zote za Shake speare.Vilevile kuna tamthiliya zilizoandikwa asilia kwa kiingereza na Waafrika kisha zikatafsiriwa kwa Kiswahili. “Maswaibu ya Ndugu Jero” na “Mzalendo Kimathi” ni mifano ya tamthiliya. Kuna tamthilia zilizoandikwa katika lugha nyingine za kiafrika na kutafsiriwa katika Kiswahili mfano wa tamthilia ni “Nitaolewa Nikipenda”.

Hivyo kwa ujumla, tunaweza kusema kuwa tafsiri ni kitendo cha kufikisha ujumbe wa matini chanzi katika matini lengwa kwa kuzingatia muundo wa lugha lengwa na maana ya lugha lengwa.

Tamthiliya ya Kiswahili ni ile tamthilia inayojadili mambo mbalimbali yahusuyo utamaduni wa waswahili na iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Mfano; “Kaptula la Maksi” yake Euphrase Kezilahabi na “Safari ya Chinga”yake Shani Omary.
Tafsiri ni nyenzo muhimu sana katika kukuza na kusambaza fasihi. Tafsiri ndilo daraja linalounganisha jamii za watu wanaotumia lugha zinazotofautiana.

 MCHANGO WA TAFSIRI KATIKA UKUAJI WATAMTHILIA YA KISWAHILI.
Kwa mujibu wa mwansoko na wenzake (2006) wanasema shughuli za wazalendo zimejadiliwa na mashirika ya utafsiri na uchapishaji ya nchi za nje ambayo yamefanya kazi kubwa ya kupanua hazina ya vitabu vya Kiswahili.
Baadhi ya mashirika hayo ni; shirika la uchapaji lugha za kigeni, Beijing China, miongoni mwa tafsiri za Kiswahili za mashirika haya ni pamoja na shajara ya mwenda wazimu na hadithi teule za lu kun.
Kutokana na maendeleo ya tafsiri fasihi ya Kiswahili imesambaa na kuwafikia watu wa mataifa mbalimbali.
Kwa mujibu wa Ruhumbika, (1978) anasema kuwa waandishi wengi wamejifunza mbinu za uandishi wa tamthiliya kutoka mataifa mengine. Mfano wa mbinu hizo ni kama vile mtindo, ujenzi  wa wahusika na uundaji na ubunifu wa mandhari na mbinu nyinginezo za kisanaa.
Mbinu hii tafsiri imefanya fasihi ya Kiswahili kukua na kuweza kuendelea kufanyiwa ulinganisho na fasihi nyingine za ulimwengu, mfano: tamthiliya ya “Amezidi” ya Said A. Mohamed. Mfano wa kazi zilizotafsiriwa; aliyeonja pepo, nitaolewa nikipenda yake ngugi wa thiong’o,” Adui wa Umma “na “Orodha”.

 Vilevile tafsiri imesaidia kuendeleza fasihi ya Kiswahili na utamaduni wake katika jamii tofautitofauti kwa mfano, kuna kazi za fasihi ya Kiswahili zikiwemo tamthiliya za Kiswahili zilizotafsiriwa ambazo ni pamoja na; “Tufani” ya Samweli S. Mushi, “Shetani Msalabani”, “Mtawa Mweusi”na “Nitaolewa nikipenda” zake Ngugi wa Thiong’o.

Pia taaluma ya tafsiri imesaidia kuongezeka kwa machapisho mengi ya kazi za Tamthiliya, hii imefanyika hasa mara baada ya kazi nyingi za tamthiliya kutafsiriwa kutoka lugha nyingine nakutafsiriwa katika lugha ya Kiswahili,mfano wa kazi zilizo tafsiriwa na kuongeza idadi kubwa ya machapisho ni pamoja na “Adui wa Umma”,”Mkaguzi wa serikali” na “Nitaolewa nikipenda”.kazi zote hizi zimesaidia katika kuendeleza ukuaji na kusambaa kwa tamthiliya.

Pia tafsiri inakuza lugha ya fasihi husika, kupitia tafsiri msamiati mpya unaingia katika lugha husika tukijua kuwa lugha ndio mhimili wa fasihi, kwa hiyo msamiati ukiimarika fasihi pia huimarika.
‘Lugha nyingi za kiafrika Kiswahili kikiwa miongoni mwao hazikuwa zimeendelea sana kimaandishi hasa maandishi ya kufasili, kwa hiyo tafsiri za tamthilia zikilenga kukuza maandishi ya lugha za Kiswahili. Na vilevile tamthilia ilitafsiri kwa lengo la kuongeza machapisho ya fasihi ya kiswahili’’ (Ruhumbika 1978).

Method (2015) anasema kuwa kazi za tafsiri zina mchango mkubwa sana katika ukuaji wa fasihi ya Kiswahili,tamthilia ikiwemo. Fasihi ya kiingereza inaonekana kunufaika sana kutokana na tafsiri ya fasihi za Kiyunani, Kiroma, Kirusi na Kifaransa (Wafula 1999:13) Ryanga (1985) katika makala yake iliyoitwa  vitabu vya kutafsiriwa na fasihi ya Kiswahili. Anasema kuwa tafsiri ina dhima kimaudhui na kifani katika fasihi ya Kiswahili na fasihi nyinginezo. Kimaudhui anabainisha kuwa aina mpya ya maudhui huweza kuibuka katika fasihi lengwa. Kifani anazitaja faida za kazi za tafsiri katika fasihi ya Kiswahili kuwa ni pamoja na kuibuka kwa mitindo mipya ya uandishi na kuingia kwa tanzu mpya katika fasihi ya Kiswahili.

 Faida nyingine tunazoweza kuziongezea hapa ni pamoja na kutia shime na kuendeleza uandshi wa kifasihi, kupanua hadhira ya kazi ya fasihi,kuongeza msamiati wa lugha na kadhalika. Kabla ya kuzama sana na kuweza kubainisha na kuchambua kazi za tafsiri katika tamthilia ya Kiswahili ni vema kwanza tufafanue kwa kina dhima hizi za tafsiri.

Tukianza na dhima ya kimaudhui, tumesema kwamba tafsiri imeweza kuibua aina mpya ya maudhui. Hii ina maana kuwa kazi inapotafsiriwa kutoka jamii lugha ambayo imepiga hatua kubwa kimaendeleo kunakuwa na maudhui mapya ambayo yanaweza kuingizwa katika fasihi lengwa hivyo kuweza kuamsha ari ya kimapinduzi. Kwa mfano inapotokea jamii yenye ukandamizaji wa wanawake ila haina mwamko wa kupinga ukandamizaji huo wa wanawake, jamii lengwa huwez kupata mwamko na kujifunza kwamba kukomeshwa kwa ukandamizwaji wa wanawake ni jambo linalowezekana.

Kwa upande wa dhima za kifani, tunaona kwamba kazi za tafsiri katika fasihi ya Kiswahili huweza kuibua mitind mipya ya uandishi. Jamii huweza kutofautiana na huweza pia kuwa na mitindo mbalimbali ya utunzi na uandishi wa kifasihi. Hivyo, kazi ya fasihi inapotafsiriwa kutoka jamii moja kwenda nyingine, jamii lengwa hunufaika na mitindo ya uandishi iliyopo katika jamii chanzi. Katika tafsiri uzingalifu wa mitindo ni jambo la muhimu sana.(Mwansoko na wenzake 2006).

Pia tafsiri huweza kusababisha kuingia kwa tanzu mpya katika fasihi lengwa. Kama inavyobainishwa na wataalamu mbalimbali, tanzu za fasihi hutofautiana kutoka jamii moja kwenda nyingine (Samwel 2012, Samwel na wenzake 2013). Hivyo kazi fulani ya fasihi inapotafsiriwa kutoka katika jamii moja kwenda nyingine ambayo haina utanzu husika, jamii lengwa hunufaika kwa kuweza  kupata aina  mpya ya utanzu. Fasihi ya Kiswahili kwa mfano imenufaishwa sana na utanzu wa tanzia ambao umeingizwa katika fasihi hiyo kutokana na kazi za tafsiri za kifasihi kama vile Oedipus the king (Sophocles) ambayo imetafsiriwa Kiswahili, Maflme Edipode ((S. Mushi).

Katika dhima ya kutia shime na kuendeleza uandishi wa kifasihi tunaona kuwa tafsiri imeweza kuwatia moyo waandishi na kuweza kuandika zaidi. Mwandishi wa kifasihi anapoona kuwa kazi yake imetafsiriwa katika lugha nyingine na kuoana hadhira pana, hummotisha kutunga zaidi. Aidha kutokea mwandishi akaandika kazi yake ya fasihi na kukosa soko katika jamii aliyoikusudia kutokana na sababu kama vile kukosekana kwa mwamko wa usomaji, umaskini, ukosefu wa elimu na kadhalika. Katika hali kama hiyo, mwandishi husika atanufaika na soko la nje kutokana na tafsiri na hivyo kutokata tama kuandika zaidi.

Dhima nyingine tuliyobainisha ni kupanua hadhira ya kazi ya fasihi. Kazi ya fasihi napotafsiriwa hupanua hadhira ya kazi ya kifasihi. Kazi hiyo hupata hadhira pana zaidi na hivyo maudhui yake kuwafikia watu wengi zaidi kuliko kama isingetafsiriwa katika lugha nyinginezo. Maudhui ya kazi ya fasihi huwalenga watu, hivyo, kama kazi husika itakuwa na hadhira finyu, mchango wa kazi hiyo katika ukombozi wa jamii huwa mdogo pia.

Vilevile tafsiri huongeza msamiati wa lugha. Husemwa kwamba jamii lugha hutofautiana katika mambo mbalimbali ikiwa pia ni utamaduni wa kiwango cha maendeleo kilichofikiwa. Kazi ya fasihi ya jamii iliyopiga hatua kubwa kimaendeleo inapotafsiriwa, huweza kusaidia jamii lugha yenye maendeleo duni kuongeza msamiati. Msamiati wa lugha hutegemeana na kiwango cha maendeleo kilichofikiwa. Lugha ya Kiswahili imenufaika sana na kazi hizi za tafsiri. Pia hudaiwa kuwa lugha kama haitumiki haikui, hivyo kutafsiri kutaifanya lugha itumike hivyo kukua.
  

 HITIMISHO.
Hivyo basi kazi ya tafsiri ni nyenzo kubwa katika kuenezana kukuza faasihi ya Kiswahili zikiwemo tamthilia ya Kiswahili kwani kutokana na kazi ya kutafsiriwa kutoka lugha mbalimbali huifanya lugha hiyo ikue kwa kuongeza misamiati na idadi ya watumiaji pamoja machapisho ya kifasihi ambayo hupelekea kukua na kuendelea kwa fasihiya Kiswahili.


MAREJELEO.

Catford J.C (1965). A linguistic translation theory of: An easy in applied linguistics. London: Oxford press.
Method, S.(2015).Umahiri Katika Fasihi ya Kiswahi, Mwongozo Kwa Mwanafunzi na Mwalimu   wa Fasihi Simulizi na Andishi. Meveli Publishers (MVP).
Mwansoko H.J.M na wenzake (2006). Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na mbinu. Dar-es-salaam: TUKI.
Ruhumbika, G. (1978). Tafsiri za kigeni katika ukuzaji wa fasihi ya Kiswahili. Makala.
Wafula, R.M (1999).Uhakiki wa tamtiliya, Historian a maendleo yake . Nairobi Kenya: Jomo Kenyatta Foundation.


TAGS:
KISWAHILI
RELATED POSTS
TAMTHILIA YA KISWAHILI
TAMTHILIA YA KISWAHILI
July 16, 20160
Historia ya tamthilia ya Kiswahili nchini Tanzania tangu kuanza kwake hadi hivi sasa
Historia ya tamthilia ya Kiswahili nchini Tanzania tangu kuanza kwake hadi hivi sasa
June 12, 20163
KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA MOFOLOJIA NA FONOLOJIA
KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA MOFOLOJIA NA FONOLOJIA
May 30, 20162

Fasili ya neno kileksika, kimuundo na kisarufi
NEXT
Fasili ya neno kileksika, kimuundo na kisarufi


DHANA YA UUNDAJI WA MANENO:
PREVIOUS
DHANA YA UUNDAJI WA MANENO:

1 comment:

UNKNOWN
16 July 2020 at 07:58
Be gentle with me. Be sweet ad kind, oh hell! Who am I kidding? Flip me over, ride my ass and pull my hair!. Hey, i am looking for an online sexual partner ;) Click on my boobs if you are interested (. )( .)Reply

 
SWAHILI LAB TV

DICTIONARY / KAMUSI
DICTIONARY / KAMUSI
SWAHILI BIBLE
SWAHILI BIBLE
FACEBOOK

QURANI TUKUFU
QURANI TUKUFU
POPULARRECENTCOMMENTS
DHANA YA UUNDAJI WA MANENO:
DHANA YA UUNDAJI WA MANENO:
11:24:0010
UNYAMBULISHAJI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
UNYAMBULISHAJI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
10:57:005
DHANA ZA MSINGI ZA MOFOLOJIA
DHANA ZA MSINGI ZA MOFOLOJIA
10:23:008
 Swali; kinzanisha Taaluma ya Isimu maana, Isimu Amali na Isimu Kokotozi.
Swali; kinzanisha Taaluma ya Isimu maana, Isimu Amali na Isimu Kokotozi.
09:47:004
BAIKOKO DANCE FROM TANGA TANZANIA
BAIKOKO DANCE FROM TANGA TANZANIA
13:11:000
TAGS
ADVANCED SWAHILI
HADITHI/STORI
KISWAHILI
SWAHILI FORUM
CUSTOM WIDGET
RECENT IN SPORTS
Created By Sora Templates & Blogger Templates
Share This :
...