Friday, 3 January 2020
JADILI MAENDELEO YA LUGHA YA KISWAHILI NADANI YA AFRICA MASHARIKI
MAREJEO
Maganga, C (1997) Historia ya Kiswahili. Dar-es-salaam. Chuo kikuu huria.
Massamba na wenzake (1999) Sarufi Miundo Kiswahili Sanifu Sekondari na Vyuo: Dar-es-salaam TUKI.
Massamba, D. (2002). Historia ya Kiswahili. Nairobi: The Jomo Kenyata Foundation.
Masebo, J. A (2002) Kiswahili Kidato cha 3 na 4. Dar-es –salaam Nyambari Nyangwine Publisher.
Msokile, M (1992) Historian a Matumizi ya Kiswahili. Dar-es-salaam: Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.
Kuku na kuenea kwa luga ya kiswahili ndani ya jumia ya afrika mashariki kumechangiwa shughuli mbalimbali katika vipindi na nyakati tofauti tofauti hivyo basi tunapo zungumzia kukua na kuenea kwa lugha ya kiswahili ndani ya jumuiya ya afrika mashariki lazima tuzungumzie chimbuko la lugha ya kiswahili pamoja na njia zilizo tumika pammoja sughuli zilizo changia kukuza lugha ya kiswahili kuanzia kipindi cha kabla ya kufika kwa wakoloni pammoja na kipindi cha utawala wa wakoloni na baada ya uhuru .
Chimbuko la lugha ya kiswahili Neno chimbuko lina maana ya mahali kitu au jambo lilipoanzia. Ama kuhusu suala la mahali hasa ambapo ndiyo chimbuko la lugha ya Kiswahili wataalamu wanahitilafiana. Wengine wanadai kuwa lugha ya Kiswahili inatokana na Kingozi lugha ya kaskazini mashariki mwa Kenya, na wengine wamesema kuwa Kiswahili chimbuko lake ni Kishomvi kilichozungumzwa na watu wa Bagamoyo na Mzizima eneo linalojulikana kwa jina la Dar –es Salaam hadi Kilwa.Wengine wanadai kuwa baadhi ya wabantu walifanya maskani yao ya kudumu katika mabonde ya kaskazini mwa mto Tana. Kikundi hiki cha wabantu ndicho kinasadikiwa kuwa chimbuko la Kiswahili katika mabonde hayo, wabantu walianzisha makazi yao Shupate naShungwaya.Mnamo miaka 500 AD, makazi ya mto Tana yalivamiwa na kushambuliwa na kabila la Wagala. Uvamizi huu uliwafanya wenyeji wake kukimbia na kusambaa katika sehemu mbali mbali za pwani ya bahari ya Hindi.Lakini ikumbukwe kwamba kuna wakazi ambao walikuwa wakiishi maeneo mbali mbali katika upwa wa Africa mashariki waliokuwa wakizungumza lugha zao mbali mbali. Lakini kwa kuwa lugha hizo zote zilikuwa za Kibantu zilikuwa hazitofautiani sana. Sasa basi, katika kuwasiliana wao kwa wao katika masuala ya kibiashara wasemaji wa lugha hizo mbali mbali walilazimika kurahisisha lugha zao kwa kiasi fulani ili waweze kuelewana na wenzao katika kurahisisha lugha zao hizo katika maeneo mbali mbali kukazuka lugha moja iliyoeleweka kwa watu wote wa eneo hilo.Hali hii ilitokea katika sehemu yote ya upwa wa Afrika mashariki kuanzia kaskazini hadi kusini. Matokeo yake yakawa ni lugha ambazo baadaye zilikuja julikana kama lahaja za kiswahili. Hivi ndivyo ilivyotokea lahaja ya Kibajuni Kitikuu katika sehemu za kusini mwa Somalia hadi kaskazini mwa Kenya. Kisiu sehemu za Pate, Kiamu katika Lamu, Chichifundi, Kimvita .Katika sehemu za Mombasa, Kivumba, Kimtang’ata katika sehemu za pwani ya kaskazini mwa Tanzania, Kimakunduchi, Kihadimu, Kitumbatu katika sehemu za Unguja na Pemba n.k. Hilo ndilo lilikuwa Chimbuko la lugha ya Kiswahili kama tuijuavyo leo.Ukizichunguza kwa makini lahaja hizo za Kiswahili ni dhahiri kuwa ni lugha kamili zinazojitegemea. Vile vile lahaja hizo zinafanana zaidi na lugha nyingine za Kibantu kuliko zinavyofanana na lahaja ya Kiswahili sanifu ambayo ina maneno mengi ya kigeni.
kuku kwa lugha ya kiswaili kabla ya uhuru
kukua kwa lugha ya kiswahi kabla ya uhuru kulitokana na shughuli walizo zifanya wakoloni kipindi chautawala wao ndani ya nchi za afrika mshariki mathumuni yao ayakuwa kukuza lugha ya kiswahili bali nikwamasilahi yao na malengo yao ikiwa ni pammoja na kuraisisha utawala wao kama ifuatavyo
Kiswahili kabla ya uhuru wageni walikitumia Kiswahili katika nyanja za elimu. Elimu ilitoa mchango mkubwa katika kipindi cha ujio wa wageni. Mfano tanganyika katika kipindi cha Wajerumani waliiteua lugha ya Kiswahili kuwa itumike kama lugha ya kufundishia na pia kusomwa kama somo la kawaida katika shule za msingi. Baadhi ya shule hizo ni kama vile Tabora, Mpwapwa na kadhalika. Hivyo walimu na wanafunzi walijifunza lugha ya Kiswahili katika shughuli za elimu sambamba na kuifanya lugha hiyo kukuwa na kuenea katika maeneo tafauti. Waarabu nao walikitumia Kiswahili ili kufundishia watoto uislamu. Hivyo misamiati mingi ilipatikana kupitia elimu. Mfano neno Madrasa, daftari, kalamu na kadhalika ambayo hadi leo yanatumika katika lugha ya Kiswahili.
Shughuli ya usanifishaji Pia wageni walisanifisha lugha ya Kiswahili. wakiwa na malengo yao tofauti tofauti ikiwemo kuweka urahisi katika shughuli ya ukusanyaji wakodi pia walitak kuwepo kwa hati moja itakayo tumika ndani ya makoloni yao Baada ya kuteuliwa kwa lahaja ya kiunguja 1930 Waingereza waliunda chama cha usanifisa wa lugha ya kiswahili juhudi mbali mbali zilifanywa katika kueneza Kiswahili mwanzoni mwa miaka ya 1930 na vita vikuu vya pili vya dunia, Waengereza walifanya juhudi za kukisanifisha Kiswahili na kukuza istilahi zake. Mfano maneno kama “Skuli”, “Shati” nk.. Hivyo Kiswahili kilitumika katika shughuli rasmi sambamba na kuenea sehemu tafauti za afrika ya mashariki.
Vile vile Kiswahili kilitumika katika nyanja za biashara.Wageni walipofika katika pwani ya Afrika Mashariki waliwakuta wenyeji wakizungumza lugha ya Kiswahili. Hivyo walilazimika kutumia lugha ya Kiswahili ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano katika biashara zao. Katika kuhakikisha biashara inakuwa vizuri Waarabu walianzisha vituo vya biashara kama vile Ujiji, Tabora n.k sambamba na kuenea kwa lugha ya Kiswahili katika sehemu tafauti na kupata mawanda mapana ya kimatumizi na watumiaji wengi.
Shughuli za kilimo Hata hivyo walikitumia Kiswahili katika shughuli za kilimo. Miongoni mwa mambo yaliyopelekea maendeleo ya Kiswahili katika kipindi cha ujio wa wageni ndani ya nchi za africa mashariki ni kilimo. Mfano Wajerumani walianzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara kama vile katani huko Tanga na kahawa huko Kilimanjaro na Bukoba. Hivyo waliajiri idadi kubwa ya vibarua kutoka sehemu mbali mbali za nchi na lugha iliokuwa ikitumika ni Kiswahili. Hivyo Kiswahili kilikuwa na ongezeko la watumiaji na kufanya lugha hiyo kuenea katika maeneo tafauti
Shughuli za kidini kadhali katika kipindi hicho dini zote mbili Ukiristo na Uislamu ni miongoni mwa sababu zilizosaidia kwa kiasi kikubwa kukuza na kueneza Kiswahili nchini KENYA, TANZANIA,UGANDA,BURUNDI NA RWANDA. ujio wa waarabu pamoja na wamisionari ulichangia sana kukua na kuendelea kwa lugha ya kiwahili ndani ya nchi za afrika mashariki kutokana matumizi ya lugha ya kiswahili katika mahubiri yao vilevile wanadini wa toa mchango mkubwa sana katika maendeleleo ya sarufi ya lugha ya kiwahili . mfano Edward stere aliandika kitabu cha sarufi ya kiswahili
Pia vyombo vya habari vilijishughulisha sana katika kueneza na kukuza lugha ya Kiswahili. Vyombo hivyo ni kama magazeti na radio. Miongoni mwa magazeti yaliyojishughulisha sana na uandikaji wa Makala mbali mbali yanayohusu lugha ya Kiswahili ni kama Msimulizi (1888), Habari za mwezi (1894), Pwani na Bara (1910) Rafiki yangu (1890), Habari leo (1954), Kiongozi (1950) Mwangaza ( 1923), Sauti ya pwani (1940) na Mazungumzo ya Walimu wa Unguja (1954) n.k. Baadhi ya magazeti hayo kulikuwa na ukurasa maalumu unaohusu taaluma ya lugha ya Kiswahili. Gazeti Mambo leo liliandika mashairi na hadithi mbali mbali za fasihi simulizi. Kwa upande wa redio Tanganyika ilianzisha matangazo yake kwa kutumia lugha ya Kiswahili mnamo miaka ya 1950. Wakati wote redio iliendelea kutangaza matangazo yake kwa Kiswahili. Hii kwa kiasi kikubwa ilichangia kukuza na kueneza Kiswahili Tanzania pamoja na nchi nyingine za afrika mashariki.
Yafuatayo ni maendeleo ya lugha ya kiswahili baada ya uhuru ndani ya nchi za afrika mashariki Baada ya nchi za Afrika Mashariki kupata uhuru (Tanganyika 1961, Uganda 1962, Kenya 1963 na Zanzibar 1964 baada ya Mapinduzi, kila nchi ikawa na kipaumbele chake katika sera ya lugha. Nchini Tanganyika na Kenya, Kiswahili kilitumika kujenga umoja na kilifanywa kuwa ni lugha ya taifa kwa nchi hizi maendele ya lugha ya Kiswahili baada ya uhuru yalitokana nashuguli na juhudi mbali mbali zilizo fanyika na wadaau kutoka ndani ya nchi za jumuiya ya afrika mashariki juudi zilizo fanyika katika kukuza lugha ya kiswahili . mfano Harakati zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania zilipelekea maenedeleo makubwa ya lugha ya Kiswahili. Mnamo mwaka 1964 lugha ya Kiswahili iliteuliwa kuwa lugha ya Taifa. Lugha hii ilitumika katika shughuli zote za kitaifa. Massamba na wenzake (2004) “ mikutano yote iliyohusiana na wananchi mijini na vijijini iliendeshwa kwa lugha hii ya taifa”. Hivyo Kiswahili kilihimizwa kutumika katika mawasiliano yote hususani katika shughuli za umma na Wizara zote pamoja na Bunge.
Jambo jengine lililopelekea maendeleo ya lugha ya Kiswahili baada ya uhuru ni kuudwa kwa tasisi na vyombo mbali mbali vya kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani ya jumuiya ya afika mshariki . Vyombo hivyo vilikuwa na majukumu makubwa kama vile kuendeleza usanifishaji lugha, kuunda istilahi na kutaarisha viiarida na vitabu ambavyo viliweza kusaidia waswahili na wale ambao wanifunza lugha ya Kiswahili. Mfano wa vyombo hivyo ni BAKITA, TAKILUKI, BAKIZA, BAMITA, UWAKIVITA pamoja na CHAKIKE nchini Kenya na kadhalika. Vyombo hivi vilisaidia sana maendeleo ya Kiswahili kutokana na kazi zao kwa kila chombo (Massamba na wenzake 2010) Kuanzishwa kwa vyombo mbali mbali vya habari viliendelea kutumia Kiswahili kwa kiasi kikubwa vyombo hivyo ni magazeti, majarida, radio, na runinga. Ambavyo vilitangaza kwa lugha ya Kiswahili. Mifano ya redio hizo ni kama radio Nuru, Adhana, Radio one, Redio Free Afrika n.k. Mifano ya runinga ni ITV, Star TV. ZBC, TBC na nyenginezo.
Shughuli za kibiashara ndani ya nchi ya jumuiya ya afrika mashariki kuhusaidia kuenea na kukua kwa kiswahili kutokana na kuwepo kwamakabila tofauti tofauti ambapo wafanyabiashara huweza kuunganishwa kwa lugha ya kiswahili.Hivyo kiswahili hudumishwa na kutumika katika biashara hizo.
Shughuli ya uandishi wa vitabu Kuibuka kwa waandishi wa vitabu mbalimbali vya kiswahili vya sarufi na fasihi ambavyovili chambua kwa kina mambo mabalimbali yahusuyo lugha ya kiswahili na utamaduni wake,mfano : Nkwera,Shabani Robart, Mathias Mnyapala na Shaffi Adam Shaffi. Waandishi wengine chipukizi walijitokeza na wanaendelea kujitokeza katika tasnia hii ya uandishi wa vitabu.hivyo imekuwa ni miongoni mwasababu iliyo changia kukuna kuenea kwa lugha ya kiswaili ndani ya jumuiya ya afrika mashariki.
Shughuli burudani (Muziki) zimechangia kueneza kukuza na kuendeleza lugha ya kiswahili ndani ya nchi za jumuiya ya nchi za afrika mshariki Shughuli hizo zimechangia sana katika kukua na kusambaa kwa lugha ya kiswahili kutokana kuingizwa kwa misamiati mipya pamoja lugha ya kiswahili kufikia jamii yote wanao penda muziki
Elimu ya watu wazima ambayo huwajumuisha watu wazima kusoma na kuandika.Watu hawa hujifunza kiswahili nakupelekea kuweza kusoma nakuandika na kuzungumza kwa lugha ya kiswahili fasaha. Masamba (2010) anasema “nchini kote elimu ya watu wazima imefundishwa kwa kiswahili kupitia masomo tofauti kama vile ufundi, siasa, kilimo, na afya. Hali hii ilisaidia maendeleo makubwa ya Kiswahili hapa nchini. Licha ya hayo maendeleo ya Kiswahili yanakuwa na kuenea sehemu mbali mbali kwa kupitia shughuli za biashara, shughuli za kisiasa, uchapishaji wa vitabu vya sarufi na fasihi, shughuli za utamaduni pamoja na harakati mbali mbali.
HITIMISHO
Ukuaji na ueneaji wa Kiswahili duniani Msokile, M (1992) anadai kuwa lugha ya Kiswahili hivi sasa imepenya sehemu nyingi duniani. Kiswahili kinazungumzwa Afrika Mashariki nzima, Somalia, Msumbiji, Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Angola, Zaire, Zambia, Ruwanda, Burundi, Nigeria, Sudan na Misri. Nje ya Afrika kuna vyuo vikuu, vituo vya redio na televisheni vinavyoshughulikia lugha ya Kiswahili. Mfano wa vituo vya redio ni Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran katika nchi ya Iran, Redio ya China Swahili, BBC Swahili London. Inasemekana hivi sasa kuwa kuna watu zaidi ya milioni 1000 wanzungumza Kiswahili duniani. Ushahidi wa hayo tunaona kuwa Papa John wa pili alitembelea Tanzania mnamo tarehe 1/06/1990 alitumia lugha ya Kiswahili. Pia Kiswahili sasa kinaendelea kutumika katika kutafsiri nyaraka mbali mbali, mitandao au tovuti, sharia, biashara, na uhakiki wa maandishi kuanzia wakati huo hadi sasa.
MAREJEO
Maganga, C (1997) Historia ya Kiswahili. Dar-es-salaam. Chuo kikuu huria.
Massamba na wenzake (1999) Sarufi Miundo Kiswahili Sanifu Sekondari na Vyuo: Dar-es-salaam TUKI.
Massamba, D. (2002). Historia ya Kiswahili. Nairobi: The Jomo Kenyata Foundation.
Masebo, J. A (2002) Kiswahili Kidato cha 3 na 4. Dar-es –salaam Nyambari Nyangwine Publisher.
Msokile, M (1992) Historian a Matumizi ya Kiswahili. Dar-es-salaam: Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.
Share This :
comment 0 Comment
more_vert