Monday, 27 January 2020
MAANA YA LUGHA
UTANGULIZI
Lugha imewahi kufafanuliwa kwa jumla kama mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa zinazotumiwa na watu wa jamii Fulani wenye utamaduni unaofanana kwa madhumuni ya mawasiliano katika jamii hiyo.
Wataalamu wengi wa isimu (sayansi ya kuchanganua lugha na kuieleza jamii) kamusi ya kiswahili sanifu TUKI 1981 oxford press uk. 86 na lugha wanaelekea kukubaliana kwamba lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumini ya mawasiliano kati yao ( massam ba D.P.B na wenzake 1999, TUKI).
Lakini inaeleweka ya kwamba viumbe vingine navyo vinaweza kutoa sauti za aina mbalimbali na aghalabu kwa madhumuni hayo hayo ya mawasiliano viumbe hivyo vinaweza kuwa kuku, amwonapo mwewe kuna lugha au sauti anayoitumia kuashilia hatari Fulani ama mbuzi anapokuwa na mtoto .
Cha kujiuliza hapa ni je, hizi nazo zinaweza kuitwa lugha? Aidha binadamu na viumbe vingine huweza kutoa ishara mbalimbali kwa madhumuni ya mawasiliano. Hizi nazo zimekuwa zikiitwa lugha kutokana na dhima yake ya kuwezesha mawasiliano baina ya viumbe hivyo swali linalohitaji kuulizwa tena katika hatua hii ni je ni kweli hizi zote ni lugha kwa maana ile ile?
Ili kujibu swali hili pengine ni muhimu kwanza kubainisha missingi ya tofauti kati ya lugha hizi zilizotajwa msingi mkubwa wa tofauti baina ya hizi “lugh” ni jinsi utoaji na utumiaji wa sauti na ishara husika vinavyochochewa kwa mfano inajulikana kwamba wakati binadamu kwa kiasi kikubwa hujifunza kutoa na kutumia sauti na ishara viumbe vingine vyote hutegemea mno silica zao katika kutoa na kutumia sauti na ishara. Hii ndio pengine ndio sababu humchukua mtoto wa binadamu takribani miaka mitatu kuweza kumudu lugha.
AINA ZA LUGHA
Wataalamu wamefikia kutenga aina kuu mbili za lugha. Hizi ni lugha asili na lugha unde.
Lugha asili ni ile inayohusisha mfumo wa sauti zinazotolewa kwa kutumia ala katika chemba yam domo wa binadamu.
Lugha unde kwa upande mwingine ni ile inayohusisha mfumo wa ishara anazobuni binadamu na ambazo huzitoa kwa viungo vyake vya nje kama vile mikono vidole kope za macho maandishi na vile vile nyenzo mbali mbali alizoziunda.
Lugha asili ina sifa ambazo unde haina hizi ni pamoja na:
kiwango cha msingi kinachohusisha vipashio kamili vyenye maana kama vile maneno na,
kiwango kingine kinachohusisha vipashio ambavyo vyenyewe havina maana lakini hutumika katika kuunda vipashio vya msingi vipashio hivi ni sauti katika lugha.
Sifa ya uzalishi kwa upande mwinginwe inahusu hasa uwezo wa binadamu wa kuunda na kuelewa idadi isiyo kikomo ya maumbo ya maneno na sentesi katika lugha yake. Hii ni pamoja na hata zile sentensi ambazo hazijawahi kutuingwa hapo kabla mifano ya uzalishi ni kama vile kutumia idadi Fulani tu za sauti kuunda maneno kadhaa kwa mfano kwa kutumia sauti t, a na o katika mipangilio mbalimbali Kiswahili upata maneno kama ota, toa tao sauti kama hizi huweza pia kuandamana na sauti nyingine katika mipangilio mbalimbali kutoa maneno mengine kama vile tako, toka, tokeza,pato,topa n.k na hadi leo hii hatujui lugha ya mnyama yeyote au lugha unde yenye sifa hizi.
Aidha sifa hizi zinazidi kutubainishia vipengele muhimu vya kitu “lugha” na kutudokeza kwamba pengine si kila njia ya mawasiliano ni lugha kwa maana ile ile.
Kwa kumalizia katika sehemu hii tumejifunza kwamba lugha inaweza kuainishwa katika makundi makuu mawili.
Lugha asili ambayo ni mfumo unaohusisha mpangilio wa sauti zinazotolewa kwa ala zilizomo kwenye chemba yam domo wa binadamu.
Lugha unde ambayo ni mfumo unaohusisha ishara zilizobuniwa na binadamu ambazo aghalabu hutolewa kwa viungo vya nje vya mwili na kwa nyenzo zilizoundwa na binadamu
Sifa kuu za
(a) (i) ni viwango viwili katika muundo wake na.
(ii) uwezo wa kuzalisha idadi isiyokikomo ya maumbo na miundo.
Sifa kuu za (b) kwa upande mwingine ni.
kuwa za idadi na aina mbalimbali kutegemea matumizi, na,
kutojulikana au kutomhusu kila mtu katika jamii.
CHIMBUKO LA LUGHA
Inawezekana kwamba kila jamii ina hadithi kuhusu jinsi lugha yake ilivyozuka. Lakini kuna hadithi kadha wa kadha kuhusu chimbuko la lugha asili zote za binadamu. Hadithi mojawapo maarufu ni ile ya biblia kuhusu vurumahi zilizotokea wakati wa ujenzi wa mnara wa babeli na kupelekea kuzuka kwa lugha nyingi. Hata hivyohadithi kama hii hata kama ina chembe ya kupelekea kuzuka kwa lugha nyingi. Haiwezi kutetewa kwa hoja za kitaalamu. Pengine hizo ziliwafanya watu walioishi babeli kutengana na kuhamia sehemu mbali mbali. Hiyo ingezusha lahaja na baadaye lugha tofauti. Kama si kwa hoja kama hii hadithi hii si chochote kitaalamu. Mnomno tutaishia tu kusema kwamba tunaamini hivyo jambo ambalo halisaidii kitaalamu.
Katika taaluma ya isimu msemo
“chimbuko la lugha “ huwa unatazamwa kwenye msingi wa fahiwa mbili kuu. Kwanza ni ile fahiwa inayozingatia hali za mabadiliko ya binadamu toka kale na kale hadi kupata lugha asili ambazo zote ni kamili na vilevile changamani kwa kiwango kinacholingana. Katika fahiwa hii pia huzingatiwa tofauti kati ya lugha asili na mifumo mingine ya mawasiliano kama ilivyoelezwa juu. Kinachoingiza mtafaruku katika fahiwa hii ni ule ukweli kwamba lugha uweza kuzuka, kukua na kufa. Fahiwa ya pili inayoongoza mtazamo wa kiisimu kuhusu chimbuko la lugha ni ile inayozingatia jinsi watoto wanavyoipata lugha. Hapa ni dhahiri kwamba hakuna mtoto anayezaliwa akiwa na lugha au na uwezo wa kusema lugha Fulani tu na si nyingine. Badala yake kila mtoto anayezaliwa akiwa na lugha au na uwezo wa kusema lugha Fulani tu na si nyingine. Badala yake kikla mtoto wa kawaida anazaliwa bila lugha lakini akiwa na uwezo wa kupagta lugha yeyote ya jamii inayomlea au inayomzunguka. Aidha ili kupata lugha ni muhimu kwa mtoto kuwa miongoni mwa jamii ya watu. Haijajulikana mtoto huathilika vipi kuhusiana na lugha pale anapotokea kuwa peke yake tu mahali popote pale.
VIPENGELE MUHIMU VYA LUGHA ASILI YA BINADAMU.
Katika ufafanuzi uliotolew kwenye utangulizi mwanzoni lugha ilihusishwa na vipengele kadha kama vile “mfumo wa sauti” “sauti za nasibu” “sauti za kusemwa” “sauti za watu wa jamii yenye utamaduni mmoja n.k
Mfumo wa sauti
Katika lugha asili zote za binadamu mifumo ya sauti ujumuisha aina mbili kuu za sauti ambazo ubainishwa kutokana na jinsi sauti hizo zinavyotamkwa. Aina kuu ya kwanza ni sauti zinazojulikana kama “irabu”au “vokali” aina kuu ya pili ni sauti zinazojulikana kama “konsonanti”
“irabu” au “vokali” ni sauti zinazotamkwa bila kuwepo kizuizi kwenye mkondo wa hewa mdomoni. Kwa kawaida tofauti katika utamkaji wa sauti hizi huletwa kutokana na mdomo kubiringwa au kulegezwa na vile vile mahali zinapotamkwa sauti hizo ambako huwa ni juu au chini nyuma mbele au katikati ya chemba. Irabu ni sauti zinazowakilishwa na herufi kama vile a,e,i,o,u
konsonanti kwa upande mwingine ni sauti zinazotamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa katika sehemu na kwa namna mbalimbali kwenye chemba yam domo. Ala kuu katika uzuiaji huu ni ulimi ambao huweza kugusishwa aju kufanywa ukaribie sana sehemu za mdomo kama vile kaakaa, ufizi, meno n.k
konsonanti nyingine hutamkwa kwa kubana mdomo na/au pua. Aidha kuna konsonsnti zinazotokea na mguno. Konsonanti zinazotokea na mguno ni zile zinazowakilishwa na herufi kama b, d, g, n.k na zisizotokea na mguno ni zile zinazowakilishwa na herufi kama f, t, s , n.k
sauti za nasibu.
Idadi na aina za sauti ambazo hatimaye hutumika katika lugha ya jamii hazipatikani kutokana na jamii yenyewe kunuia au kukusudia hivyo. Ama kwa hakika huwa hakuna vikao wala mikakati maalumu ya jamii yenyewe kunuia au kukusudia hivyo. Ama kwa uhakika huwa hakuna vikao wala mikakati maalumu ya jamii kukubaliana kuhusu sauti hizo. Jammi hujikuta tu ikitumia sauti hizo ambazo, kwa kawaida huweza kutofautiana kidogo tu au sana na zile za jamii nyingine hali hii ya sauti za lugha kupatikana bila wenyewe kunuia au kukusudia ndiyo huitwa nasibu.
Unasibu huonekana pia katika uundaji wa maneno na tungo mbalimbali katika lugha. Kwa mfano huwa inatokea tu kuwa mpangilio wa sauti Fulani kwa namna Fulani kama vile katika umbo maji huunda neon hilo ambalo jamii ya waswahili hulitumia hulitumia kuita aina Fulani ya kioevu. Kitu hicho hicho huitwa kwa maneno yenye maumbo tofauti kabisa katika lugha nyingine. Maumbo haya ni kama vile water (katika kiingereza) eau (katika kifaransa), pi ( katika kiluo), ma “(katika kiarabu), amanchi (katika kihacha), n.k imetokea tu kwa jamii hizi zinatumia maneno haya kuita kitu hicho na hakuna anayeweza kudai kwamba neon lake ndilo hulandana na kitu hicho kuliko maneno ya jamii nyingine.
Sauti za kusemwa
Maelezo kuhusu vipengele vilivyotangulia yanasisitiza umuhimu wa sauti katika lugha asili ya binadamu jinsi zinavyotolewa na vile vile kupangika kwake hadi kuunda maneno na sentensi. Aidha imedhihirika kwamba huwa kuna utoaji wa sauti na utoaji tu wa sauti na utoaji wa sauti kwa mpango maalum. Aina ya kwanza ya utoaji wa sauti mara nyingi hauna maana yeyote na hivyo kwa kawaida hauhusishwi na kitu “lugha” aina ya pili ya utoaji wa sauti ambayo ujulikana pia kama “kusema” ndiyo sifa maalumu ya lugha asili, na kwa hakika ndiyo sifa kuu inayobainisha lugha asili ya binadamu na “lugha” nyinginezo. Aidha kitendo cha kusema ndicho huwa cha mwanzo katika mfululizo wa taratibu za upatikanaji wa lugha na matumizi yake. Taratibu nyingine kama vile uandishi na matumizi ya ishara nyingine hufuata baadaye na si kwa watu wote katika jamii. Ni dhahiri pia kwamba hizi njia nyingine haziwajkilishi lugha kikamilifu. Kwa mfano, hadi leo hii hakuna mfumo wa uandishi unaowakilisha lugha kikamilifu kabisa. zaidi ya kushindwa kwa njia hii kuwakilisha sauti zote kwa namna inayorizisha, huwa pia haitoi nafasi kwa vipengele vingine vya lugha kama kiimbo, shadda n.k . hii ndiyo imefanya wataalamu mbalimbali duniani kuita lugha ya kusema kuwa ndiyo lugha ya msingi. Taratibu nyingine kama vile uandishi huwa ni za kujaribu tu kuwakilisha lugha hii ya msingi.
Sauti za watu wa jamii yenye utamaduni mmoja.
Lugha inafungamana sana na na jamii ya watu. Na kwa kuwa lugha huwa ni kwa ajili ya mawasiliano yote katika jamii, ni dhaili kuwa inabeba na kuakisi mambo mengi ya jamii husika. Mambo mbalimbali ya jamii ndiyo huwa kiini cha utamaduni wa jamii hiyo. Utamaduni hujumuisha mambo kama fikra na falsafa ya jamii na vile vile namna mbali mbali jamii inavyoendesha mambo yake. Aidha kuna ukweli kwamba lugha ndiyo msingi mkuu wa ubunifu ( wa fikra na mambo mengine) na wa utoaji wa maelekezo vitu ambavyo ni muhimu kwa jamii yoyote ile. Zaidi ya hayo lugha katika maumbile yake fulani Fulani huweza kudhihirisha vipengele vinavyoakisi msimamo au mtazamo wa jamii juu ya mambo mbalimbali. Kwa mfano uainisho wa majina ya vitu katika lugha mbalimbali hudhihirisha mitazamo tofauti ya jamii yenye lugha hizo kuhusu vitu hivyo. Wakati mathalani lugha kama kifaransa, kiarabu na nyinginezo huainisha majina ya vitu kwa msingi wa kijinsia (yaani kama cha kike ama cha kiume) lugha nyingine kama zile za kibantu huainisha vitu kwa msingi wa dhana mbalimbali tofauti.
HISTORIA YA KISWAHILI
Katika kamusi ya Kiswahili sanifu (TUKI 1980), historia inafafanuliwa kama elimu maalumu ya matukio yaliyopita . kwa maana hiyo historia ya kitu chochote ni elimu maalum ya matukio yanayohusu kitu hicho tangu wakati muda mfupi au mrefu uliopita. Hii inafanya iwe muhimu katika elimu hii, kwanza kuamua matukio ya kushughulikiwa yawe ni yale ya kuanzia lini. Kwani inawezekana mathalan, kutoa historia ya kitu tokea kale kabisa au kuanzia kipindi Fulani hadi kipindi Fulani tu. Vile vile huwa ni muhimu kuamua kuwa historia hiyo ikidhi malengo gain. Malengo ya jumla ya historia huwa:
kuelewesha tu hali ya mambo ilivyokuwa hapo kabla nap engine kuhusisha hali hiyo na hali ya sasa au ya baadaye,
kujulisha sababu, namna na hali ya matukio, au
kujulisha hali ya sasa kwa kutazama yaliyotokea nyuma.
Zaidi ya maelezo hayo ya jumla ya historia huwa ipo pia haja ya kujiuliza umuhimu wa historia ya lugha. Utakumbuka kwamba katika muhadhala wa kwanza, lugha ilifungwa mno na jamii ya watu kutokana na kubeba kwake vipengele vya utamaduni wa jamii inayohusika nakutoa taswira ya mienendo yake. Ama kwa wanafasihi, lugha inachukuliwa kuwa “kioo cha jamii” katika hali kama hii, historia ya lughahuweza kuelimisha kuhusu:-
vipengele mbalimbali vya lugha yenyewe katika kipindi kirefu cha kuwepo kwake, na
hali na mambo ya jamii yenye lugha hiyokama vile asili yake, jinsi inavyotazama dunia n.k.
na kwa kuwa jamii na lugha hubadilika yawezekana pia kubainisha sababu, namna na hali ya mabadiliko hayo katika historia ya lugha.
Kumekuwa na nadharia kadhaa kuhusu chimbuko la lugha ya Kiswahili. Hizi ni pamoja na nadharia kwamba lugha hii ina asili ya kiarabu na nadharia kwamba lugha hii ni mchanganyiko wa lugha ya kiarabu na za kibantu. Lakini kwa kuwa hizi ni nadharia tu ni jukumu letu katika muhadhara huu kuthibitisha ni ipi kati yake ina mashiko zaidi.
Nmadharia inayohusisha Kiswahili na kiarabu imetokana na mambo kadhaa mawili makuu. La kwanza ni jina la lugha hii ambalo kwa wakati huu, linakubalika kwamba linatokana na neno la kiarabu sahil na wingi wake sawwahil lenye maana ya upwa/ pwani. La pili ni idadi ya msamiati wa Kiarabu uliomo katika Kiswahili. Shina Swahili lilijitokeza katika maandishi kwa mara ya kwanza mnamo karne ya 14 lilipotumiwa na mwanazuoni mmoja maarufu wa kiarabu aliyejulikana kwa jina la Ibn Batuta. Mwanazuoni huyu alitumia neno hili kuelezea hali hali ya eneo la kijiografia na maumbile ya kijamii na kitamaduni ya pwani ya afrika ya mashariki aliyokuwa ameitembelea. Jina la kiarabu lenye maana ya “pwani” kutumiwa kuita eneo na mambo ya pwani ya afrika mashariki, bila shaka ni muafaka. Lakini je kutumika kwake hivyo kunatosha kufanya liashirie kwamba Kiswahili kina asili ya kiarabu au mahusiano ya kiarabu na lugha hiyo? Ili kudhihirisha asili ya kitu ni lazima pia kutazama vipengele vingine kadhaa. Kwa kitu kama lugha vipengele hivyo huweza kuwa mambo kama na muundo wa lugha na vilevile zana za kitamaduni zinazobenwa na lugha hiyo kama tulivyoona katika muhadhara wa kwanza. Jina tu halitoshi kudhihirisha asili ya kitu. Kwani katika bara la afrika hasa matumizi ya majina ya kkuita watu, mahali na vitu kwa kiasi kikubwa, yamekuwa kiholela hata kufanya yasipate uzito unaostahiki kuthibitisha kitu. Kwa mfano majina kama ziwa Victoria, ziwa Albert, n.k yana nini kuhusu asili na yalipo maziwa haya? Je majina ya watu ya kusilimu nay a ubatizo?
Idadi ya msamiati wa kiarabu katika Kiswahili, kwa upande mwingine nayo ina historia ya wazi ambayo ni dhahiri haifikii kugusa masuala ya msingi kuhusu asili ya lugha hii. Jambo hili itabidi tulieleze kwa kutazama, kwa ufupi, historia ya ujio wa wageni Afrika mashariki na athari zake.
Pwani ya afrika ya mashariki ilitembelewa na baadaye kukaliwa na kukaliwa na wageni kadha wa kadha kutoka sehemu za asia na ulaya kwa muda mrefu sana. Wageni hawa ambao ushahidi wa kufika kwao umo hata katika waraka wa karne ya kwanza uliojulikana kama periplus of Erythrean Sea, waliingiliana na wenyeji hata kuathiriana nao kwa kiasi Fulani. Kwa kuwa hapo mwanzoni wageni hawa walikuwa wachache , athari yao ilikuwa haipo au ndogo. Idadi ya wageni, hasa kutoka bara arabuni, iliongezeka hasa baada ya karne ya saba kutokana na luja za uhamiaji zilizochochewa na ujio wa harakati za kujikita kwa uislamu huko. Tokea hapo, shughuli kama biashara, harakati za kueneza dini na maingiliano ya kawaida ya kijamii ambazo ziliendelea kwa kiasi kidogo huko nyuma, zilipamba kasi hata kupelekea sehemu za pwani ya afrika ya mashariki kuingia chini ya mamlaka za masultani wa kiarabu. Hali hii iliendelea kwa karne nyingi na ilikuja kuingiliwa tu na wareno mnamo karne ya kumi na sita na vilevile wazungu wengine kuanzia karne ya kumi na tisa. Wazungu hawa baadaye walianzisha tawala zao toka pwani hadi bara tawala ambazo zilidumu hadi takriban miongo mitatu tu iliyopita.
Karne nyingi wageni walizoishi na kutawala pwani ya afrika mashariki zilishuhudia kuongezeka kwa athari ambazo zilikumba pia lugha za pwani. Kuongezeka kwa msamiati wa lugha za kigeni katika lugha hizi ni sehemu ya athari hizo. Cha kujiuliza katika hatua hii ni je, msamiati hasa wa kiarabu katika Kiswahili ni mkubwa kiasi ganihata kufanya uchukuliwe kuwa ushuhuda wa asili ya lugha hii?
Hadi leo hii waandishi hutofautiana katika makadirio yao ya msamiati wa kiarabu uliomo katika Kiswahili. Kwanza makadirio haya ambayo ni kati ya asilimia 20 na asilimia 40 yametokana mno na vyanzo vilivyoandaliwa na wageni wenyewe kama vile orodha mbali mbali za maneno na kamusi. Pili utafiti wa hivi karibuni (Bosha 1993 :1) unaonyesha pia kwamba msamiati mwingine ambao umekuwa ukichukuliwa kuwa wa kiarabu kumbe unatoka katika lugha nyingine. Lakini cha muhimu ni kwamba, hadi leo hii tafiti nyingi hazijazingatia hali ya lugha uswahilini kwenyewe. Kwa mfano orodha za bosha (kur 31, 32) zinzhusu nyanja kama vile utawala sheria, dini, biashara n.k ambazo zimekuwa katika dhana za kigeni. Kwa kiasi kikubwa makadilio yote juu yamekuwa yakitegemea msamiati katika nyanja hizi bila juhudi kufanyika kuchunguza kama uswahilini kuna msamiati mwingine unaotumika badala ya huo wa kigeni. Zaidi ya hayo, Kiswahili kina mazingira yake mengine mapana yenye idadi kubwa ya msamiati asilia ambayo huwa haitiliwi maanani katika makadilio hayo. Ieleweke kuwa nia hapa si kukana kuwepo kwa msamiati wa kigeni katika Kiswahili bali kuonyesha kwamba pengine idadi yake imekuwa kupita kiasi katika hali kama hiyo ni dhahiri inahitaji tahadhari kuhusisha idadi hiyo ya msamiati wa kigeni na asili ya Kiswahili.
Kiswahili ni kibantu.
Inajulikana kwamba lugha ambayo, leo hii tunaiita “Kiswahili sanifu” msingi wake ni kiunguja, mojawapo ya lugha ya kienyeji kisiwani unguja. Kutokana na unguja kuwa kituo muhimu cha misafara ya kibiashara kwenda na kutoka bara lugha ya mahali hapo ndiyo ilitumiwa katika misafara hiyo. Hali hiyo iliipatia kiunguja fursa ya kuenea katika sehemu nyingi za bara, sifa iliyoiwezesha kuchaguliwa kama msingi wa lugha sanifu wakati wa usanishaji wa lugha mnamo mwaka 1930.
Leo hii kiunguja na lugha nyinginezo za mwambao wa afrika mashariki, huitwa”lahaja” za Kiswahili kutokana na mahusiano ya karibu kati yake. Hii ina maana kwamba hizi zote ni lugha ndogo ndogo zenye tofauti kieneo na vile vile asili moja ya kundi mama liitwalo “Kiswahili” kwa makosa kundi hili mama hili limekuwa likichukuliwa na watu wengi kuwa ndicho Kiswahili sanifu. Ukweli ni kwamba Kiswahili sanifu ni kizalia tu cha miongo ya karibuni. Lakini kwa kutazama kipindi lilipoanza kutumika jina “Swahili” ( yaani karne 14 au kabla ) inawezekana bado kuchukulia kundi mama la lugha hizi kuwa “Swahili”
Dhana ya kundi mama la lugha nyingi imeitwa “mame lugha” (Chiragndin 1974:57) na imetumika sana katika isimu linganishi kuchunguza historian a mahusiano ya jamii za lugha. Umuhimu wa dhana hii ni kuonyesha hatua za kuzaliana kwa jamii za lugha toka kale. Uchunguzi wa mahusiano haya ya kuzaliana hukihusisha Kiswahili na kundi mama liitwalo “mame-sabaki” (nurse 1978 :173) mame-sabaki ni mama wa makundi ya lugha za kibantu yajulikanayo kama sabaki. Pokomo. Mijikenda na Ngazija. Ushahidi wa kiakiolojia na kiisimu unaonyesha kwamba “mame-Swahili” imetokana na kundi la sabaki na yawezekana ilijitenga mnamo karne ya kumi (Nurse(1987) zaidi ya haya mahusiano ya kihistoria lugha ya Kiswahili , hadi leo hii, pia bado inaonyesha mahusiano ya karibu na lugha nyingine za kibantu katika vipengele mbali mbali. Hivi n pamoja na taratibu za uambishaji na unyambulishaji, ngeli za majina na dhana zinazoandamana nazo, orodha ya msamiati wa msingi n.k hapa chini tunatoa mifano michache ya mfanano wa baadhi ya vipengele kati ya Kiswahili na kihacha (lugha ya kibantu iliyoko katika ufuko wa mashariki wa ziwa viktoria, yapata kilomita 1000 kutoka pwani ya Bahari ya Hindi).
Kiswahili kihacha
A.UAMBISHAJI
m-tu o-mu – ntu
wa – tu a – ba – ntu
a – na – kunywa a – ra – nywa
tu – na – kula tu – ra – ria,
B.NGELI A MAJINA
M - /WA - MU -/BA-
M -/MI - MU -/MI-
JI -,Q -/MA- RI -,KU-/MA
KI -/VI- KI -/BI-
N -/N- N -/N-
Katika sehemu hii tumejifunza kwa muhtasari, masuala mbalimbali kuhusiana na chimbuko la Kiswahili. Haya ni pamoja na nadharia kuhusu asili ya Kiswahili. Imedhiirika kuwa zile nadharia zinazohusisha asili ya Kiswahili na kiarabu hazina mashiko. Badala yake Kiswahili kinaonyesha, toka kale hadi leo hii, mahusiano thabiti na lugha nyingine za kibantu. Mahusiano haya, zaidi ya kuonekana wazi wazi kwenye maumbile ya lugha wakati huu, yanathibitishwa pia na ushahidi mbalimbali wa kiakiolojia na wa kiisimu.
Kuenea kwa Kiswahili
Kiswahili kilienea kagtka sehemu nyingi ndani ya bara kutokana na shughuli mbalimbali za watu. hapo
awali, shughuli hizi zilikuwa ni zile za biashara, utawala na utangazaji wa imani za dini. Kwa kiasi kikubwa, shughuli hizi ziliendeshwa na wageni ambao waliongoza misafara ya wabeba mizigo, walinzi na wakalimani kutoka na kurejea pwani. Katika njia za misfara hii nako kulianzishwa vituo mbalimbali ambako baadaye zilijengwa makanisa/mjisikiti, makao makuu ya utawala wa shule. Kutokana na shughuli zilizoendeshwa humo, vituo hivyo navyo baadaye vilikuwa vitovu vya maenezi ya lugha na mambo mengine.
Harakati za kukieneza Kiswahili pia hazikuwaacha nje ujerumani ambao katika kipindichao kifupi cha utawala Tanganyika walianzisha shule zilizotoa elimu kwa kuswahili. Ni dhahiri malengo ya utawala wa kijerumani Tanganyika wakati huo ilikuwa ni kuwapata watumishi wa ngazi za chini kwa ajiri ya shughuli za utawala. Hatua hii ya kuwafunza na kuwatumia watu kama hawa ilisaidia katika kueneza lugha.
Utawala wa wajerumani ulifuatiwa na ule wa waingereza. Hatua kubwa iliyochukuliwa na waingereza kuhusu Kiswahili ni kuundwa kwa kamati ya lugha ya afrika mashariki iliyokuwa na jukumu la kusanifisha lugha. Kazi hii ilifanyika mwaka 1934 na kamati ikabakia na kazi ya kufuatilia maendeleo ya lugha sanifu. Hata hivyo, katika mfumo wao wa elimu waingereza walisisitiza matumizi ya lugha yao ya kiingereza na kuinyima Kiswahili sanifu fursa ya kutosha katka karibu sehemu zote rasmi. Matumizi ya Kiswahili wakati wa utawala wa waingereza yalipamba kasi tu wakati wa harakati za kudai uhuru.
Katika kipindi cha cha utawala wa wajerumani na kile cha utawala wa waingereza kulikuwa na juhudi nyingine kadha wa kadha zilizosaidia kukieneza Kiswahili. Hizi ni pamoja na kuanzishwa kwa vitabu na magazeti yatolewayo kwa Kiswahili katika sehemu mbalimbali, vituo vya utangazaji kwa njia ya redio na kuingia kwa vyombo vya kukata na kupiga santuri. Hizi ni hatua ambazo zimezidi kupanuka hadi hii leo. Lakini hatua kubwa na muhimu kuliko zote iliyochukuliwa baada ya kupatikana uhuru ni ile ya kukitangaza Kiswahili kama lugha ya taifa Tanzania na Kenya. Hii ni hatua ambayo hadi leo hii haijachukuliwa kuhusiana na na lugha yeyote ile ya kiafrika. Hatua hii ilichukua hatua mpya ya ufungamano kwa lugha hii kipindi baada ya kupatikanika uhuru Tanzania pia ilishuhudia hatua za kuundwa kwa vyombo mbalimbali vya kustawisha lugha. Hivi ni pamoja na vyombo rasmi kama vile baraz ala Kiswahili la taifa (BAKITA) Taasisi ya uchunguzi wa kiswahili (TUKI) na idara ya Kiswahili ya chuo kikuu cha Dar es Salaam.Hatua ya muhimu inayosubiriwa ni ile ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya mafunzo katika ngazi za juu za elimu.
MATUMIZI NA MABADILIKO YA KISWAHILI
Lugha kama chombo muhimu cha jamii inayotofauti zake mbalimbali kama ilivyo jamii yenyewe. Tofauti hizi huweza kuongezeka au kupungua kjulingana na harakati mbalimbali zinazoendelea katika jamii husika. Uthibitisho wa tofauti katika lugha ni ule wa kuwepo kwa lahaja mbalimbali za lugha moja na tofauti nyingine miongoni mwa wasemaji. Aidha lugha kama jamii, inaweza kukumbwa na mabadiliko mbalimbali yanayoweza kuiathiri kwa kiasi kikubwa au kidogo. Katika historia ya Kiswahili tuliona athari au mabadiliko yaliyoikumba lugha ya Kiswahili hata kufikia kuwakanganya watu kuhusu asili yake. Mabadiliko haya yalipelekea lugha yenyewe kupewa jina la kigeni na vilevile kuingiziwa maneno mengi ya kigeni kutokana na kuwepo wageni katika mazingira yake.
Tofauti na mabadiliko katika lugha, kimsingi, ni tofauti na mabadiliko katika matumizi yake. Hii hutufikisha kwenye lahaja ya kujiuliza nini maana ya matumizi ya lugha. Matumizi ya lugha ni jinsi hasa lugha inavyotumika katika mazingira/miktadha mbalimbali kutegemea hali nyingi za watumiaji wa lugha hiyo na vile vile za mazingira/miktadha hiyo. Kwa mfano Kiswahili kina tofauti ya usemaji wake baina ya watumiaji wa maeneo yake ya kaskazini na wale wa maeneo yake ya kusini. Hali hii ndio huzua tofauti za kilahaja, yaani tofauti kulingana na maeneo lugha inakosemwa. Lugha hii vilevile inatofauti baina ya matumizi yake katika muktadha rasmi na yale katika muktaza usiokuwa rasmi. Zaidi ya hayo matumizi ya lugha huweza kutegemea hali mbalimbali za watumiaji wake kama vile umri, jinsia elimu, uchangamfu, uoga, haya n.k. mambo haya na mengine mengi huchangia katika kuathiri jinsi hasa lugha inavyotumiwa na watumiaji mbalimbali. Nia katika muhadhara huu itakuwa ni kusisitiza kwamba japokuwan lugha inatumiwa kwa namna hizo mbalimbali bado inao mfumo fasaha wa matumizi ambao ndio kipimo cha mawasiliano bora miongoni mwa watumiaji wake wote.
KANUNI NA TARATIBU ZA MSINGI
Kabla ya kuzungumzia tofauti na mabadiliko mbalimbali yanayojitokeza katika matumizi ya lugha ya Kiswahili, pengine ni muhimu kutaja kwamba lugha hii kama lugha nyingine yoyote inazo kanuni na taratibu mbalimbali za msingi ambazo ndizo huongoza matumizi yake. Uzingatifu wa kanuni na taratibu hizi za msingi ndio kwa kawaida huchukuliwa kama kigezo cha matumizi bora ya lugha. Kanuni na taratibu hizi vilevile ndizo msingi wa kuelewana lugha miongoni mwa waumiaji wote. Lakini lugha pia huwa zina taratibu zisizo za msingi zinazoruhusu upambaji au uremaji wa maelezo ili kufikisha ujumbe kwa namna inayokidhi hali na mazingira ya mawasiliano. Taratibu hizi ni kama vile sifa za kiarudhi, mitindo ya utamkaji na utumiaji wa maneno na vilevile uundaji miundo, uchaguzi na matumizi ya maneno aina aina n.k kwa kawaida, taratibu hizo zisizokuwa za msingi hukumbwa sana na tofauti na mabadiliko aina aina miongoni mwa watumiaji wa lugha. Jumla ya tofauti na mabadiliko yanayoweza kutokea kutokana na mwanya kwenye taratibu zisizokuwa za msingi yanaweza kuainishwa katika misingi mine mikuu. Hizi ni:
. msingi wa kieneo
.. msingi wa mukktadha/mazingira ya
matumizi.
… msingi wa hali za watumiaji na
…. Msingi wa athari za lugha za jirani.
TOFAUTI ZA KIENEO
Lugha huwa inatofauti kulingana na maeneo walikosambaa watumiaji wake. Huu ndio msingi wa lahaja za lugha ambazo huakisi tofauti katika lugha moja kulingana na maeneo inakosemwa, hali hii huwa ni matokeo ya kawaida ya utengano baina ya watumiaji wa lugha. Hali hii vile vile ni matokeo ya lahaja ya kukithi matakwa ya mazingira mahsusi.
Lugha ya Kiswahili inazotofauti za kieneo. Tofauti hizi zinzdhihirika katika lahaja zake ambazo ni nyingi. Hadi sasa idadi kamili ya lahaja hizi haijulikani, lakini baadhi ya wandishi (polome 1967), walifikiria zinaweza kufika 18 lahaja hizi zimeenea pwani na kisiwani kutoka eneo kaskazini mwa msumbiji. Kwa upande wa kusini, hadi huko Somalia kwa upande wa kaskazini. Mifano ya lahaja ya Kiswahili ni kama vile kiunguja, kimvita, kitumbatu, kimtang’ata, kivumba, chimiini, kipate, kiamu, kingwana n.k. kila moja ya lahaja hizi ina tofauti zake lakini ambazo hazisababishi kukwama kwa maelewano baina ya wasemaji wake na wale wa lahaja nyingine. Tofauti kama hizio zinapozidi katika lahaja moja hadi kusababisha kukwama kwa maelewano na lahaja nyingine, basi lahaja kama hiyo itakuwa imepata hadhi ya kuwa lugha tofauti. Hii ndiyo hali ambayo pengine inajitokeza baina ya baadhi kubwa ya lugha za kibantu.
Kwa jumla kuna tofauti za wazi baina ya lahaja za Kiswahili za maeneo ya kaskazini na zile za maeneo ya kusini. Tofauti hizi ni za kifonolojia , kimofolojia na kimuundo (au kisintaksia). Mifano ya tofauti za ni kama vile kutumika kwa sauti nd, t n.k. kaskazini wakati kusini hutumika nj n ach badala yake katika maneno kama ndoo/njoo,tini/chin ink. Mifano ya kimofolojia, kwa upande mwingine, ni kama vile maumbo ya majina kama uele/ndwele “kaskazini hali kusini hutumika maumbo uele/maele. Mifano mingine ni kama vile maneno mayi/maji,uu/juu,twaa/chukua, n.k. na mifano ya tofauti za kimuundo ni kama vile kikimbizwa kaskazini, hali kusini hutumika kinachokimbizwa, n.k.
Tofauti kama hizi na nyingine nyingi ndizo zilizopelekea kuwepo kwa haja ya lugha sanifu inayoweza kuwahudumia watumiaji wote.
MUKTADHA/MAZINGIRA YA MAELEZO
Muktadha na mazingira ya matumizi ya lugha nayo uchangia katika kuwepo kwa tofauti za aina nyingi ndani ya lugha miktadha au mazingira kama hayo ni mengi. Baadhi yake ni kama vile muktadhi rasmi na ule usiokuwa rasmi. Muktadhi rasmi wa matumizi ya lugha ni ule uneohusu shughuli za serikali au nyinginezo ambazo huwa zinawekewa kumbukumbu. Muktadha usiokuwa rasmi kwa upande mwingine ni ule unaohusu maongezi yeyote ya mitaani au kwingineko ambayo hayawekewi kumbukumbu na hayalazimishi kuwepo kwa umakini katika utoaji wake. Aidha kuna miktadha ya sehemu za shughuli maalum kama vile uvuvi, ujenzi, ubaharia, ushauri, uandishi n.k ambako misamiati na mitindo mahsusi hutumuika katika kila shughuli. Miktadha hii ndiyo msingi wa mitindo ya matumizi ya lugha inayojulikana kama rejesta. Hivi ni vilugha vinavyotofautiana kulingana na muktadha wa shughului kama zilizotajwa. Mazingira ya shughuli Fulani hulazimisha kuwepo kwa msamiati na miundo mahsusi kwa shughuli hiyo. Kwa mfano, katika biashara ya chakula migahawani, hakuna anayeshtuka kusikia maelezo kama Nani mbuzi? Nani kuku? Nani chai? Ng’ombe mbili? N.k vivyo hivyo wavuvi, wajenzi, wasomi, n.k nao wana misamiati na mitindo mahsusi kwa nyanja zao.
ATHARI ZA LUGHA JIRANI.
Tofauti katika matumizi ya lugha huweza kujitokeza pia kutokana na athari za lugha jirani. Kiswahili mathalan, kimekwishawahi kukumbwa na athari za lugha za nje kama kiarabu, kijerumani na kiingereza na vilevile na athari za lugha jirani zake. Maelezo kuhusu athari za kiarabu juu ya Kiswahili yalijitokeza katika muhadhara wa kwanza . athari za lugha jirani nazo zinadhihirika katika orodha ya msamiati wake na vilevile katika matumizi ya wasemaji wake ambao hizo lugha jirani ni zao za kwanza. Kiswahili pia kimeathiri lugha jirani kwa viwango tofauti.
Athari za lugha jirani huweza kuwa kubwa au ndogo kutegemea shinikizo na hadhi za lugha husika. Kwa mfano, kiarabu kama lugha ya watawala wa enzi hizo ambao walijihusisha pia na shughuli nyingine kama vile biashara na uenezaji wa dini, ilikuwa na hadhi ya juu na hivyo kutia shinikizo kubwa katika Kiswahili.
Tofauti mbalimbali za matumizi ya lugha zilizojadiliwa zina athari kadha wa kadha ambazo ni muhimu zielezwe hapa. Athari hizi ni pamoja na kuwepo kwa maneno mengi tofauti yenye maana moja, neno moja lenye maana nyingi tofauti kutegemea muktadha wa matumizi, mzneno kubadilika maana katuka mazingira na vipindi tofauti, na kuingia kwa msamiati wa kigeni ambao hupata maumbo tofauti. Athari hizi zinzweza kuchangia katika kunawirisha matumizi mapana ya lugha lakini vilevile zinzweza kuzusha pingamizi katika matumizi ya lugha. Kuwepo kwa athari hizi kunaipatia lugha akiba kubwa ya msamiati, mitindo na peo za matumizi ambazo lugha sanifu huweza kuzijumuhisha ili zitumike kwa mapana zaidi miongoni mwa watumiaji wote. Na kama tulivyozoea awali pingamizi katika matumizi ya lugha huweza kutokeka pale tofauti zilizozungumziwa humu zinzpokuwa kubwa.
FASIHI KWA JUMLA
UTANGULIZI
Fasihi ni uwanja mpana unaohusisha matumizi ya lugha kisanaa. Kama tulivyoona katika muhadhara wa tatu, lugha ina matumizi yake ya kawaida katika maongezi au mazungumzo ya siku hadi siku baina ya watu au makundi mbalimbali ya watu katika jamii. Sifa moja kuu ya lugha ya maongezi au ya mazungumzo ya siku hadi siku ni kuwa si lazima ifungane na tafakuri za ndani sana na ubunifu. Hapa fikra au maoni hutolewa kadri ya mwendo na muktadha wa mazungumzo au maongezi. Hali hii ni tofauti, mathalani, na pale mtu anaposimulia hadithi watu wengine. Katika hali kama hiyo, hadithi hiyo, ikiwa ya kweli au ya kubuni, itahitajika ionyeshe mambo kadhaa kama vile matukio muhimu, mtiririko wake, mantiki ya hadithi nzima na mtiririko wa matukio ndani yake. Vile vile hadithi itahitajika kukidhi malengo Fulani kama vile kuburudisha, kuadibisha, kuelimisha n.k. matumizi ya lugha kwa kuzingatia mambo kama hayo yaliyotajwa na mengine mengi ndiyo matumizi ya lugha kisanaa. Hii ndiyo sifa kubwa ya kazi zote za fasihi ambazo ni pamoja na riwaya,tamthiliya, ushahiri,ngonjera na kadhalika.
Lakini nyanja za sanaa ni nyingi na fasihi ni mojawapo tu miongoni mwake. Nyanja nyingine za sanaa ni kama vile uchoraji, ufumaji, uchongaji, ufinyanzi, na utarizi, muziki n.k. ambazo ni dhahiri hazikitwi katika matumizi ya lugha. Nyanja zote za sanaa, ikiwa ni pamoja na fasihi zina sifa kadhaa zinazofanana. Hizi ni pamoja na sifa ya kuwa na umbo dhahiri na timilifu, ile ya kuwa kiwakilishi cha jamii na ile ya kila mara kunuiwa kufanikisha lengo Fulani. Katika muhadhara huu hatutajihusisha na hizi nyanya nyingine za sanaa. Nia yetu kuu itakuwa ni kuchunguza vipengele na dhana za msingi katika taaluma ya fasihi. Hizi zitakuwa ni pamoja na aina za fasihi, tanzu za fasihi na matumizi ya lugha katika kazi za fasihi.
AINA ZA FASIHI
Fasihi imegawanyika katika aina kuu mbili kwa kuzingatia mno jinsi inavyowasilishwa na kuhifadhiwa na si katika misingi ya tofauti kwenye maumbile ya taaluma yenyewe. Aina hizi mbili ni fasihi andishi na fasihi simulizi. Fasihi andishi ni kazi za fasihi zinazowasishwa kwa masimulizi ya mdomo na kuhifadhiwa fikirani mwa wanajamii mbalimbali.
Kumekuwepo na utata wa namna Fulani kuhusiana na uainishaji wa fasihi ulioonyeshwa juu. Utata huu unahusu hasa uliopo mpaka kati ya kazi simulizi na kazi andishi. Hii ni kwa sababu kuna kazi nyingi ambazo hapo awali zilikuwa zikisimuliwa tu lakini baadaye zikawekwa katika maandishi na vivyo vivyo kazi za maandishi ambazo zimekuwa zikisimuliwa tu lakini baadaye zikawekwa katika maandishi na vivyo vivyo kazi za maandishi ambazo zimekuwa zikisimuliwa. Aidha wapo wanaodai (taz. K.m TUMI(1988:113-117) ) kwamba kazi simulizi hata kama ikiandikwa, haibadiliki hadhi bali huwa imehifadhiwa tu kwa njia hiyo. Hii ni kwa kuwa fasihi simulizi inazo sifa zinazoibainisha ambazo ni utendaji mbele ya hadhira na vilevile uwezo wa kubadilika kulingana na hadhira. Fasihi Andishi kwa upande mwingine, japokuwa nayo huweza kuigizwa, huwa hairuhusu mabadiliko mbalimbali ya papo au ya muda mrefu kwa kuwa imejikamilisha kiandishi. Hata hivyo, uainishaji wa fasihi kama andishi au simulizi bado, kwa kiasi kikubwa, zinaendelea kutegemea kazi simulizi.
Kitu kingine ambacho pengine kingehitaji kutazamwa hapa kwa ufupi ni jinsi kazi zinavyoweza kuendelea kujidumisha mbele ya mabadiliko yote yanayoikumba jamii, imekwishaonekana, mathalan, kwamba kadri uandishi unavyoshamiri ndivyo nafasi na hadithi ya masimulizi zinavyozidi kupungua. Hii ni kwa kuwa maandishi yanaendana na mabdiliko mengine katika jamii kama vile kujua kusoma na kuandika na vilevile taratibu mpya za maisha zinazoruhusu wanajamii kuishi mbali na mazingira yao na jamii zao. Lakini maandishi vilevile hufifisha masimulizi kwa kutoweza kunakili vipengele vyote vya kazi simulizi. Inajulikana, mathalani, kwamba kazi simulizi huwa zinaandamana pia na vitendo na vitabia vya fanani (mtendaji) ambavyo huziongezea huai. Vitendo na vitabia hivyo si rahisi kujitokeza katika maandishi au katika namna nyingine za uhifadhi wa kumbukumbu kama vile picha, kanda za sauti n.k. huwa pia si rahisi kwa kumbukumbu kama hizo kusambaa kwa wanajamii wengi na kwa ubora ule ule. Haya yote huonyesha ugumu uliopo kwa fasihi simulizi kuendelea kujidumisha katiaka jamii hasa kunapokuwepo msukumo mkubwa wa mabadiliko. Hata hivyo mbele J.L (1982:1-8) anaonyesha kwamba aina hizi mbili za fasihi tayari zinaonyesha uwezekano wa kujidumisha kila moja ikinufaisha nyingine.
TANZU ZA FASIHI
Katika kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI 1980:308), neno “utanzu hufafanuliwa kama “tawi,utagaa” hiuvyo tunapozungumzia “tanzu za fasihi “ ina maana tunazungumzia matawi ya fasihi. Lakini inaonekana kuwa ipo haja ya kutenga dhana “matawi”/utanzu” na aina” za fasihi zimechanganywa (taz. K.m Msokile (1992:4,5,9 na 12 na hivyo kugawanya wasomaji. Tungependa “aina” za fasihi zilizobainishwa juu zibaki kama zilivyoelezwa. Lakini tungependa pia dhana “tanzu za fasihi “ieleweke kama maumbo mbalimbali ya kazi za fasihi (andishi au simulizi). Hizi ujulikana pia kama fani.
Tanzu kuu za fasihi ni Hadithi, Ushairi na sanaa za maonyesho. Utanzu wa hadithi unajumuisha riwaya (=hadithi ndefu), visa (=hadithi fupi) na katumani (=novella) katika maandishi na ngano, visaasili, vigano n.k. katika masimulizi. Utanzu wa ushairi, kwa upande mwingine, hujumuisha mashairi, tenzi na ngonjera. Hizi huweza kujitokeza hivyo hivyo katika maandishi na katika masimulizi. Utanzu wa sanaa za maonyesho, kwa upande wake hujumuisha tamthiliya, vichekesho, ngonjera n.k utanzu huu umejulikana pia kwa jumla kama drama.
Tanzu hizi pia zina sifa zifuatazo ambazo huzibainisha. Hadithi, mathalan, ni kazi ya fasihi inayotumia lugha ya natharia ya nadhari au maelezo ya moja kwa moja kama katika lugha ya kawaida. Aidha, hadithi huweza kuwa ya kweli au ya kubuni na hujengwa kwa kuwatumia wahusika kuelezea tukio au matukio. Ushairi kwa upande mwingine, ni kazi ya fasihi ambayo umbo lililotawalia ni lile la vina na mlingano wa mapigano ya sauti au mizani. Katika Kiswahili leo hii, kazi za ushairi zinajumuisha pia maumbo mengine yenye lugha ya mkato na yaliyogawanywa kwenye vifungu vinavyolingana au kutofautiana. Maumbo haya yote, katika ushauri wa Kiswahili yanaakisi athari za ushairi wa kiarabu na wa kizungu. Sanaa za maonyesho, kwa upande wake, kwa kuwa huwa zimelengwa kuwasilishwa mbele ya hadhira huwa zina maumbo yam kabala wa ana kwa ana baina ya wahusika. Aidha utanzu huu huwa unafungana na vipengele vingine kama vile mahali pa kutendea na mchango wa hadhira. Kazi za utanzu huu vilevile hugawanywa katika maonyesho kadhaa yanayoakisi hatua za ujenzi wa matukio hadi kwenye upeo na baadaye.
3. MATUMIZI YA LUGHA KATIKA KAZI ZA FASIHI
Uti wa fasihi ni matumizi ya lugha kisanaa. Ilidokezwa kwamba lugha inapotumiwa kisanaa ina tofauti na lugha ya kawaida.
Tashhisi, kwa upande mwingine, ni matuzi yanayovipatia uhai vitu visivyo na uhai kama katika mfano ufuatao:
“Vijito viliimba nyimbo tamu za furaha wakati vikibubujika kuelekea chini ya mlima”
aidha, takriri ni matumizi yanayorudia rudia maneno au silabi kwenye neno ili kutia mkazo au kusisitiza kitu.
Aina za tamathali
Aina maana mfano
Kejeli matumizi yaliyo
Nuiwa kutoa maana
Kinyume. Maruburage
(kihaya enye kengeza)
dhihaka matumizi yaliyobuniwa kuumiza
sitiari matumizi yanayounganisha kitu kimoja na kingine kwa kuvifanya sawa sawa. Mfano wakati ni titi la nyati hukamuliwan kwa shaka.
Tasfida matumizi yanayoficha ukali na utusi wa maana mfano mtoto yule ana mikono mirefu.
Kijembe matumizi ya kufumba papo hapo yakidokeza maana ya fumbo. Mfano mzee kifimbo.
Matumizi maalum ya lugha kama ilivyoonyeshwa katika tamathali za semi juu ndiyo matumizi ya lugha kisanaa ambayo lengo lake ni kutoa picha inayofanana au kukaribiana na hali halisi ya mambo. Matumizi haya maalum ya lugha hujumuisha pia methali, nahau n.k.
Fasihi pia ina zana nyingine za mtungo wa maneno kwa lengo la kuleta maana maalum. Hizi zinajulikana kama taswira, ishara na tanakali. Taswira (au Jazanda) ni uwasilishaji wa mawazo, dhana n.k kwa vielelezo vinavyojengwa kwa maneno. Ishara, kwa upande mwingine, ni kitu kinachotajwa kwa maana inayowakilisha dhana Fulani pana. Kwa mfano bendera huweza kutumiwa kama mfano wa utawala n.k. tanakali, kwa upande wake ni marudio rudio kama yanavyojitokeza katika vina vya ushairi, n.k. haya yote ndiyo ukamilisha jumla ya matumizi ya lugha kisanaa kwa madhumuni ya kufikisha ujumbe kwa namna maalum.
UMUHIMU WA FASIHI KATIKA JAMII
Katika utangulizi ilidokezwa kwamba kazi za fasihi huwa zimenuiowa kukidhi malengo Fulani maalum. Hizi zilionyeshwa kuwa ni pamoja na kuelimisha, kuburudisha na kuadibu jamii. Kwa kuwa fasihi inahusu maisha ya binadamu, huwa inatumia mifano halisi ili kufikisha ujumbe unaotakiwa, lengo kuu likiwa ni kumjenga mtu kifikra na kitamaduni. Aidha fasihi kama uwanja wa kitaaluma ina dhima ya kupanua peo za fikra ili kumwezesha mtu kuona mbali na kuhusisha matukio na hisia za ndani. Kazi za fasihi, vilevile zimetumiwa kisiasa na kitamaduni ili kutoa mwelekeo kwa wanajamii kujua mwenendo na mkondo wa maendeleo yao. Haya yote ndiyo hufanya kazi za fasihi zichukuliwe kama kiwakilishi au kioo cha jamii.
MISINGI YA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI
Kuhakiki kazi ya fasihi ni kuitafakari na kuichanganua kwa madhumuni ya kuzama katika peo zake zote. Lengo kuu la uhakiki huwa ni kuelewa hali halisi ya jamii, matatizo yake na utatuzi wa matatizo hayo.
Kazi ya fasihi uhakiki kwa kuchunguza vipengele vya maudhui kama vile dhamira na ujumbe na vipengele vya fani kama vile muundo, mtiririko, wahusika lugha iliyotumika n.k kinachochunguzwa ni jinsi hivi vipengele mbalimbali vilivyojengwa na kama ujenzi huo unakidhi malengo ya kisanaa nay a kufikisha ujumbe inavyopasa. Uhakiki pia huweza kuandamana na mitazamo ya kinadharia hasa kuhusu misingi ya kijamii na taratibu zake mbambali kama vile imani n.k.
SARUFI YA KISWAHILI KWA JUMLA.
UTANGULIZI.
Sarufi inafafanuliwa kama “elimu ya miundo na mfumo wa lugha ya binadamu” (khamisi 1978:5) Elimu hii inajaribu kuonyesha kanuni zinazotawala lugha Fulani, kanuni ambazo zinajulikana kwa kila binadamu mwenye kutumia lugha hiyo wakiwemo watoto wenye umri kuanzia walau miaka mitatu.
Sarufi kwa jumla inahusisha vipengele maridhawa ambavyo vimefungamana kwa karibu sana lakini ambavyo vinaweza kutengwa katika nyanja tofauti kulingana na misingi na vigezo vya kila moja ya vyanzo hizo. Vipengele hivi ni pamoja na vipashio vidogo na vikubwa na vile vile taratibu mbalimbali zinazohusika katiaka maumbo ya maneno na miundo katika lugha. Sarufi huanzia pale vitamkwa katika lugha vinapoanza kupangwa kwa namna mbalimbali kuunda maneno. Kwa hiyo, bila hata kujua mfumo wa vitamkwa hivyo vilivyo katika lugha inawezekana kudadisi kwamba maneno katika lugha ya Kiswahili kama vile zito, zika, toza toka, katiza n.k bila shaka yanatokana na mipangilio tofauti ya vitamkwa /z/,/k/,/i/,/a/,/a/,/t/,/o/. maneno kama hayo yaliyoundwa kutokana na mipangilio mbalimbali ya vitamkwa kama hivyo, hatimaye hupewa maana katiak lugha hiyo. Kwa ujumla lugha mbalimbali hutofautiana katika aina na idadi ya vitamkwa vyake na vilevile katika jinsi ya kupanga vitamkwa hivyo kuunda maneno.
Ili kuunda maneno kutokana na vitamkwa vyake mbalimbali lugha inahusisha taratibu kadha wa kadha. Kwa mfano katika lugha za kibantu uundaji wa maneno huhusisha:
(a) kanuni zinazojenga mizizi ya aina ` mbalimbali za maneno;
(b) kanuni zinazounda viambishi mbalimbali;
(c ) kanuni za kuunganisha mizizi na viambishi n.k
katika lugha hizi miziz ni vipashio ambavyo ni viini vya maneno ambavyo havigawiki katika sehemu ndogo zaidi. Viambishi kwa upande mwingine ni vipande vidogo vidogo vya semi ambavyo havijitegemei lakini ambavyo hupata umuhimu vinapounganishwa na mizizi. Maneno yanayoundwa kutokana na taratibu hizi mbalimbali huwa nayo yana tabia zake tofauti za mahusiano na meneno mengine. Tabia hizi ndizo huwa msingi wa kanuni zinazohusika katika uundaji wa miundo mipana zaidi kama vile virai na sentensi.
Vipashio na taratibu zinazopelekeakuundwa kwa maneno katika lugha hushughulikiwa na utanzu wa sarufi unaojulikana kama sarufi maumbo au mofolojia. Vipashio na taratibu zinazopelekea kuundwa kwa sentensi zinazokubalika katika lugha, kwa upande mwingine, hushughulikiwa na utanzu wa sarufi unaojulikana kama sarufi miundo au sintaksia. Tanzu hizi mbili ni miongoni mwa tanzu nne kuu za kiisimu zinazoshughulikia vipengele mbalimbali vya lugha. Kwa kuwa kila moja ya tanzu hizi una misingi na vigezo vyake vya uchanganuzi unaweza ukajitegemea ingawaje vipengele vya lugha vinashughulikiwa karibu huwa ni vile vile katika viwango na hadhi tofauti.
Tunapozungumzia sarufi kwa ujumla, kimsingi , huwa tunazungumzia vipashio na taratibu zinazoshughulikiwa na tanzu za sarufi maumbo na sarufi miundo. Sarufi huwa inahusisha kwa kiasi Fulani tu vipashio na taratibu zinazoshughulikiwa na tanzu za fonolojia na semantiki japokuwa vipengele vya lugha vinavyohusika ni vile vile kama tulivyodokeza juu.
Kwa mfano tunajua mathalan lugha ya Kiswahili ina kitamkwa /a/. kama kitamkwa katika lugha hii, /a/, kina sifa zake maalum zinazokibainisha na vitamkwa vingine . kwa mfano kitamkwa hiki ni mojawapo ya irabu katika lugha hii inayotamkwa katika sehemu ya chini ya chemba wakati midomo imelegezwa. Sifa kama hizo za kitamkwa /a/ ndizo hushughulikiwa na utanzu wa wa fonolojia. Lakini hali ya hiki kitamkwa huwa tofauti pale inapokuwa sehemu ya neno kama lala. Katika neno hili /a/ ya kwanza, ni irabu katikati ya konsonanti mbili ambavyo kwa pamoja hujenga mzizi wa neno. /a/ ya pili kwa upande mwingine ni kiambishi tamati ambacho kina hadhi tofauti. Hadhi ya kitamkwa katika muktadha wa neno hilo pia ni tofauti na hadhi yake katika muundo a- na ambako inapata sifa nyingine tofauti. Sifa za kitamkwa hiki katika muktadha wa neno kama lala ndizo hushughulikiwa katika sarufi maumbo wakati sifa zake katika muktadha wa tungo ana ndizo hushughulikiwa na utanzu wa sarufi muundo wakati sifa zake katika muktadha wa tungo ana ndizo hushughulikiwa na utanzu wa sarufi muundo. Katika kiwango cha sarufi miundo, mathalani, /a/ ya kwanza ni kiwakilishi, cha nafsi ya tatu umoja, kiambishi na katika utamkaji wa tungo hiyo, inajitegemea kama silabi. Haya ndiyo jumla ya mambo maridhawa ambayo yanajitokeza katika lugha na ambayo kama hayakutenganishwa, huwa yakiwakanganya sana wanafunzi wa lugha.
SARUFI MAUMBO YA KISWAHILI
Kipashio mzizi. Hiki ni kipashio ambacho hakiwezi kugawika katika vipande vidogo na ambacho huwa ndicho kiini cha maneno katika lugha. Mizizi katika maneno ya Kiswahili hujengwa ama kwa kitamkwa kimoja au vitamkwa kadhaa kwa kufuata kanuni Fulani maalum. Kwa mfano mizizi mingi, hasa ile inayounda aina ya maneno inayojulikana kama vitenzi, katika Kiswahili na lugha nyingine za kibantu huwa ni ile ya mfuatano wa konsonanti (k) Irabu (i) na Konsonanti (k) kama katika lal-, pat-,pik-,pig-, n.k. mizizi mingine ni ya mfuatano wa IK kama vile f- j-,l-, n.k. na ile yenye I tu kama vile o-, u-, n.k. mizizi kama hii huunda vitenzi moja kwa moja ikiongezewa kiambishi –a mwishoni. Inaweza pia kuongezewa kiambishi au viambishi nyambulishi kadhaa kuunda vitenzi vingine katika lugha hii , mizizi yenye mfuatano KI hutumika sana pia katika uundaji wa aina nyingine ya maneno inayojulikana kama majina k,m – tu, ti, -su,to- n.k. ili kuunda majina mizizi kama hii hutanguliwa na viambishi mbalimbali. Baadhi ya majina katika Kiswahili pia ina mizizi kama hii hutanguliwa na viambishi mbalimbali. Baadhi ya majina katika Kiswahili pia ina mizizi yenye mifuatano ya IKKI kama katika umba n.k. KIKI kama katika keka n.k. aina nyingine za maneno katika lugha hii huwa na maumbo kamili k.m na, zuri, ovyo, pu n.k nah ivyo kutohusisha dhana ya mizizi ya maneno.
Viambishi kwa upande mwingine, navyo ni vya maumbo mbalimbali kama tulivyokwishadokeza juu. Aidha, vipo viambishi vinavyotangulia mizizi na vile vinavyofuata mizizi kama kama ilivyoonyeshwa juu. Kwa kawaida, viambishi katika Kiswahili hujengwa kwa mfuatano wa IK au KI na vilevile kwa I au K tu kama katika –ik-, mi-, m-,-a n.k kwenye maneno kama pig- ik-a mi-ti, pand-a n.k. viambishi navyo, kama ilivyokuwa kuhusiana na mizizi, huweza kuhusika na aina Fulani tu ya maneno. Kwa mfano, katika lugha hii kuna orodha kubwa ya viambishi vinavyoambishwa tu kwenye mizizi ya majina. Viambishi hivi ndivyo hujulikana kama viambishi vya ngeli za majina . lakini vipo pia viambishi kama –ji, -fu, -vu, -o, -e, n.k., ambavyo hutumika kuunda vitenzi vingine kutokana na mizizi mbalimbali. Viambishi hivi ambavyo vinajulikana kama viambishi nyambulishi hufuata mizizi na kila moja huweza kutokea peke yake na mzizi au kuandamana na vingine kadhaa. Miandamano kama hii nayo hufuata kanuni maalum. Kwa mfano, katika mwandamano wowote –w lazima kikae mwisho, n.k.
Kwa jumla mahusiano baina ya viambishi na mizizi huongozwa na taratibu mbili kuu. Hizi ni uambishishaji (=pale viambishi vinapotangulia mizizi) na unyambulishaji (=palle viambishi vinapofuata mizizi ili kuunda maneno mengine). Tumeona pia kwamba kuna kanuni nyingine nyingi za mipangilio ya vitamkwa kuunda viambishi na mizizi au ya mipangilio ya viambishi vyenyewe. Maelezo hayo hutufikisha kwenye hatua nyingine muhimu inayohusu aina za maneno yanayoundwa kutokana na vipashio na taratibu zilizoelezwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya kihore (1995:98-109) kwanza, “neno” hufafanuliwa kama umbo dogo kabisa la usemi lililo huru, pili huonyeshwa kwamba Kiswahili kina aina nane za maneno. Aina hizi ni majina (inayotaja viumbe na vitu) vitenzi (inayotaja matendo ya viumbe na vitu), vielezi (inayotaja sifa ya matendo ya viumbe na vitu), viwakilishi( inawakilisha vityajwa halisi), viunganishi(inayounganisha neno na neno au tungo na tungo), viingizi inayotangulia maelezo, na viigizi (inayotokana na miigizo ya jinsi mambo au vitu vinavyofanyika).
Mifano:
Majina … … mtu unyama, kitabu n.k
Vitenzi … … lala, oga, ungua
Vivumishi … zuri, refu, kali
Vielezi … … kabisa, ovyo, sana.
Viwakilishi … mimi, sisi, wao
Viunganishi … na, lakini, ama
Viingizi … hebu, lo, kumbe
Viigizi … … pu, chubwi, parakacha
Baadhi ya aina hizi za maneno zimewahi kujulikana pia kwa majina mengine. Majina haya mengine yalibuniwa kulingana na vigezo walivyovitumia waainishaji. Kwa mfano, vivumishi viliwahi kujulikana huko nyuma kama sifa: vielelezi kama visifa au pia advebo: viwakilishi kama vijana: viunganishi, kama vihusishi, viigizi kama viisishi na viigizi kama vilio. Aidha, viunganishi na/aui vihusishi vimewahi kwa pamoja kuitwa miao (kopoka 1956). Vilevile majina vionyeshi na vimilikishi yamewahi kuita maneno ambayo yanajumuishwa ndani ya aina vivumishi.
SARUFI MIUNDO YA KISWAHILI
Vipashio muhimu vya kimuundo katika utanzu huu ni neno kamili au mafungu ya maneno ambayo upangika kutokana na uhusiano maalum. Kiini cha uhusiano baina ya maneno ni tabia ya “neno kuu”. Hili ni neno ambalo ndilo chimbuko la mahusiano baina ya maneno katika fungu au kirai. Uhusiano baina ya “neno kuu” na maneno mengine huwa ni ya “uchomozi”. Hii ina maana kwamba uhusiano huo unatokana na tabia ya neno kuu. Uchomozi hutokea kwa namna mbalimbali kutegemeana na tabia ya neno kuu kama inavyodhihirika katika mifano ifuatayo.
A. MTOTO = mdogo
= yule mdogo
= yule mdogoaliyezaliwa mwaka
jana.
B. SOMA = kitabu
SOMEA = juma kitabu
C. KWA = kalamu
= kaka
= uangalifu mkubwa
D.HARAKA = sana
= sana sana.
E. ZURI = sana
= sana Sana
katika mifano hii neno lililo andikwa kwa herufi kubwa ndilo neno kuu. Tabia ya kila mojawapo ya maneno hayo ndiyo uruhusu mahusiano kama yale yaliyoonyeshwa. Maneno makuu haya hayawezi yakabadilishana nafasi katika mahusiano hayo ya uchomozi. Kwa mfano, huwezi kuwa na fungu “MTOTO uangalifu mkubwa” au “HARAKA kalamu” n.k.
katika lugha ya Kiswahili. Zaidi ya hayo mahusiano haya yote ya uchomozi hayalingani kwani wakati yalle katika (B) na kwa kiasi Fulani, yale katika (c) ni ya lazima yale katika (A), (D) na (E) si ya lazima. Na, kwa hakika, katika Kiswahili na katika lugha nyingine nyingi, mahusiano ya lazima hasa kama yale katika (B) ndiyo kwa kawaida huwa viini vya sentensi katika lugha.
Miundo kama ile iliyopo katika kundi (A) inayochomoza kutokana na nomino MTOTO ndiyo huitwa kikundi Nomino katika sarufi muundo. Ile katika (B) inayochomoza kutokana na kihusishi KWA ndiyo huitwa kikundi Husishi. Aidha miundo katika (D) inayochomoza kutokana na kielezi HARAKA ndiyo ujulikana kama kikundi elezi. Miundo kama ile katika (E) kwa upande mwingine, haijawahi kubainishwa rasmi katika sarufi miundo ya Kiswahili. Miundo hii utofautiana na ile katika (D) kutokana na jinsi inavyoweza kufuatana na vipashio vingine katika sentensi. Kwa mfano, wakati miundo katika (D) huweza tu kufuata vitenzi ila katika (E), basi, bila shaka itajulikana kama kikundi vumishi. Kitakachokuwa muhimu baada ya hapo ni kuthibitisha umuhimu wa kipashio kama hcho katika Kiswahili.
Kwa hakika, msingi wa sentensi katika lugha yeyote ni mahusiano baina ya vipashio kama vile vilivyobainishwa katiaka (A) hadi (D) kwa mfano, kutokana na mafungu katika (A) hadi (D) unaweza kupata sentensi kama:
Mtoto yule mdogo anasoma kitabu kwa uangalifu mkubwa .
Mtoto yule mdogo anasoma haraka sana.
Tungependa pia tugusie kwa ufupi suala la mahusiano ya lazima kama yale katika (B) ambayo tulidokeza kwamba huwa ndiyo kiini cha sentensi katika lugha. Ikumbukwe kwamba mahusiano haya yanachomoza kutokana na vitenzi. Ingawa haikuonyeshwa katika mifano iliyotolewa juu, ukweli ni kwamba miongoni mwa maneno makuu yaliyobainishwa katika mifano (A) hadi (E) yale katika (B) ndiyo yana ruwaza za aina nyingi zaidi za mahusiano ya uchomozi. Mahusiano haya ni baina ya neno kuu na shamirisho yake/zake. Tunaweza tukafafanua shamirisho kama kipashio chenye mahusiano ya lazima na neno kuu kuitofautisha na kijalizo ambacho kina mahusiano ya hiari na neno kuu. Mahusiano ya lazima huwa kama ifuatavyo: unapotumia kitenzi kama vile somea katika sentensi anayekusikiliza atatarajia ukamilishe maelezo yako kwa kutaja anayesomewa na anachosomewa. Bila vipashio hivyo viwili kujitokeza sentensi yenye kitenzi hicho haiwi kamili. Kutokana na mahusiano kama haya, vitenzi huunda ruwaza nyingi ambazo ndizo huwa viini vya sentensi katika lugha. Hapa chini tutaonyesha ruwaza mbalimbali zinazotokana na tabia tofauti ya makundi ya vitenzi ruwaza hizi tutazionyesha kwa utaratibu ufuatao. Katika (a) tutaonyesha kanuni ya mahusiano husika katika (b) mifano ya aina ya vitenzi husika na katika (c) mfano wa muundo husika.
1. (a) T2 - T.
(b) kufa,kupigana, n.k.
(c) a-m-e-kufa.
2. (a) T2 – T, N2
(b) andika, vaa, somewa, n.k.
(c) a-na-andika barua.
3. (a) T2- T,N2, N2.
(b) pa, nyima, pigia, n.k.
(c) a-me-mnyima mtoto chakula.
4. (a) T2 – T, T1.
(b) panda, taka, amua, n.k
(c) a-na-penda kusoma
5. (a) T2 – T, E, T1
(b) kuwa
(c) i-ta-kuwa vizuri kumwona.
6. (a) T2 – T, N2,T1
(b) fundisha, omba, lazimisha, n.k.
(c) a-me- m-lazimisha juma kula.
7. (a) T2 – T(kwamba/kuwa)s
(b) sema,lalamika n.k.
(c) a-me-lalamika(kwamba)amepunjwa.
8. (a) T2 – T, N2,(KWAMBA/KUWA)S
(b) ambia, agiza, omba n.k.
(c) a-me- ni- ambia(kwamba) atarudi.
9. (i) (a) T2 – T,V
(b) kuwa
(c) ni mzuri
(ii) (a) T2 – T, H2
(b) kuwa, kuja
(c) a-li-kuwa na pesa
alikuja kwa mikiki.
(iii) (a) T2 – T, N2 (pahala)
(b) kuwa
(c) yumo darasani.
TANBIHI T2 = kikundi tenzi
T = kitenzi(neno kuu)
T1= kikundi tenzi ngoekwa
N2 = kikundi nomino
E = kielezi
H2 = kikundi husishi
(Kwa ujumla istihala hizio ni za nadharia ya sarufi miundo virai ambazo ni tofauti na za sarufi mapokeo kama vile kiima kitenzi yambwa n.k kwa kuwa si rahisi kulinganisha istilahi hizi kikamilifu ni vema kwa kazi kuzingatia msingi wa nadharia/ mkabala Fulani tu)
mifano hii inadhihirisha kwamba kutokana na mahusiano ya lazima baina ya vitenzi na shamirisho, tunapata ruwaza ambazo ni viini vya sentensi katika Kiswahili. Kwa kuwa ruwaza hizi zote zinatokana na sifa moja kuu, yaani mahusiano ya lazima baina ya neno kuu na shamirisho, zinaweza zikachukuliwa kama viini vya sentensi sahili. Lakini itadhiohilika pia kwamba aina nyingine zote za sentensi huundwa kwa kuunganisha ruwaza hizi kwa njia na namna mbalimbali. Kwa mfano, sentensi ambatano, zinaundwa kwa kuunganisha ruwaza hizi kwa kutumia viunganishi kama na, lakini, n.k. sentensi chanmgamano nazo huundwa kwa kuunganisha ruwaza kama hizi kwa kutumia ama viambishi kama vile –po- -ki- nge- ngali- n.k au kwa kutumia maneno kama vile kama, japokuwa, ingawa, ikiwa n.k.kwa kutumia dhana ya neno kuu kama tulivyotumia hapa tutakuwa pia tumeua dhana maarufu katika sarufi ya Kiswahili kama vile kitenzi kisaidizi na kitenzi kishirikishi kwani miundo inayohusisha dhana hizi itashuighulikiwa na kanuni katika (4) juu.
Hapa imeonyeshwa kwamba tabia ya neno ndio huwa kiini cha mahusiano baina ya meneno yanayounda kirai. Mahusiano haya huweza kuwa ya lazima au ya hiyari. Mahusiano ya lazima kama yale yanayochochewa na tabia za vitenzi mbalimbali katika lugha ndiyo huwa viini vya sentensi sahihi katika lugha. Imedhihirika kuwa ruwaza za mahusiano kama hayo ni nyingi. Aidha ruwaza kama hizo zikiunganishwa kwa njia mbalimbali ndizo hupelekea kuundwa kwa aina nyingine za sentensi kama vile sentensi ambatano na sentensi changamano.
MISINGI YA ELIMU MAANA.
Nadharia ya elimu maana kuhusiana na lugha asilia ya binadamu hugawanyika sehemu mbili. Sehemu moja hujulikana kama uamali (=pragmatics) na nyingine hujulikana kama semantiki (gazdarna wenzie 1985:7) uamali hushughulikia uhusiano baina ya maelezo na vitajwa. Kwa jumla uamali huhusu mno mtazamo wa mtumiaji wa lugha hasa kulingana na vipingamizi na/au athari za kijamii za matumizi ya lugha. Mfano wa uamali hudhihirika katika sentensi kama hii ifuatayo:
Mtoto aliyezaliwa jana anaogelea. 3
Sentensi kama hii ni sahihi kisarufi ila ni wazi haikubaliki kwa wasemaji wa Kiswahili. Lakini kutokubalika kwake hakuhusiani na maana yake bali na mazoea katika jamii husika. Imekuwa kawaida kwa watumiaji wa lugha kuchukulia hali kama hii kuihusu maana kwa namna sawa na vipengele vingine vya maana katika lugha.
Ama kuhusu semantiki napo pia kuna vipengele vinavyohitaji kubainishwa. Kwanza kuna hilo suala la uhusiano wa maelezo na kitajwa kama vile mtu, mbwa, n.k. hiki kwa hakika, ndicho kipengele cha elimu maana kinachojulikana sana kwa watumiaji wengi wa lugha. Lakini kuna kipengele kingine cha elimu maana kinachohusisha maelezo na muundo mzima. Inajulikana mathalan, kwamba maana ya sentensi huwa haitegemei maana ya neno moja moja katika sentensi hiyo. Kwa kawaida muundo huwa una maana yake isiyofungana na ile ya vipashio vilivyondani yake. Aidha kuna uwezekano wa neno au muundo mmoja kuwa na maana kadhaa. Wakati kipengele cha elimu maana kinachohusu uhusiano wa maelezo na kitajwa kinatumika sana, vile kuhusu miundo havijashughulikiwa sana kitaaluma. Kumeanza tu kufanyika juhudi mbalimbali za kitaalamu za kubuni jinsi ya kufanya maelezo ya maana ya miundo.
Kifonolojia (elimu sauti)
Mofolojia (sauti maumbo)
Sintaksia (sarufi muundo)na
Semantiki elimu maana.
Orodhesha vitamkwa vya Kiswahili ambavyo ni.
ng’ong’o
vipasua
vikwamizi
SARUFI MAUMBO
VIWAKILISHI
Ni maneno yenye kusimama katika nafasi ya majina/ nomino. Kwa dhana hiyo ni maneno yawakilishayo majina, wengine huviita vibadala. Viwakilishi huweza kuwa katika fungu la mofimu huru kwani vitumikapo hujibu maswali au katika mawasiliano huria hujitosheleza kimaana, mf: yeye, kipi? Chochote na kadhalika
AINA ZA VIWAKILISHI.
(a) Viwakilishi vimilikishi
Ni mofimu zitumikazo kuonyesha umiliki wa majina tajwa kama vile kiti, nyumba, mke, mume, kalamu, chakula n.k
Mifano; kiti chake – kiti cha juma. Cha Komole n.k
Mke wetu – mke wake mke wa johno n.k
Mume wake – mume wa Fausta, n.k
(angu, ake, etu, enu, ao, a (mwalimu, Hamisi, n.k)
(b) Viwakilishi vionyeshi;
Huwa ni vile visimamavyo katika nafasi ya majina yenye kuonyeshwa mara nyingi hujulikana kutokana na upatanisho wa kisarufi (word concord/ subject verb agreement)
(-ile, -yo, -cho, -yu, -ki n.k mf; kile vile,wale,yule, zile, huyo, hayo, hicho; hiki, huyu, hao, n.k)
katika mazungumzo ya kawaida viwakilishi hivi husaidiana na vidoko vya mwili.
(c) viwakilishi viulizi
maneno/ mofimu zitumikazo kuuliza majina ya vitu, watu hali, mahali, n.k
yupi, wapi, kipi, nani, nini, lini n.k (mfano kitu gani, mtu gani n.k)
(-pi, -ni).
(d) Viwakilishi vya O- rejeshi; (-o-, -ye-, -vyo-, -cho-, n.k) (virejeshi)
Hivi ni viambishi vinavyoambatanishwa kabla ya mzizi wa kitenzi kuonyesha urejeshi. Mfano; waliOtumwa wamerudi, watakaOenda waseme, kiliCHOpotezwa kimelipwa, aliYEdanganya asikabidhiwe madaraka, mnaOsoma.
(e) Viwakilishi vya –ote na –o-te/ -e-ote
Huwakilisha jumla ya majina ya kundi moja mf; wote, vyote yeyote, vyovyote, chochote, chote , lote, lolote, n.k.
Vimenunuliwa vyote, Amekimaliza chote, Nipe lolote, Anaweza kwenda popote, fanya vyovyote vile n.k.
(f) Viwakilishi vya –enye.-enyewe.(viwakilishi nafsi)
Hivi huwakilisha majina yenye kujitaja kama vile mimi “mwenyewe” au mimi ni mwenye nyumba hii n.k
Mifano; Lile lenye kelele limeshapita.
Mwenyewe hakuwahi kunieleza habari hiyo.
Kilicholetwa ni chenyewe kabisa.
Watoto wenyewe wakorofi kama mama yao (au baba yao)
VIVUMISHI
Sarufi mapokeo ilivifanya visifa/ au maneno yatoayo sifa za majina. Baadae ilionekena kuwa si vivumishi vyote vitoavyo sifa ya majina.
Vivumishi ni kipashio ambacho hutoa maelezo zaidi juu ya jina/ nomino. Vivumishi vya kiswahili huweza kuambikwa mizizi yake na hivyo mara nyingi huweza kuwa mofimu huru au tegemezi. Mf zuri, baya, dogo (hizini mofimu huru). –vu, -fu, (tovu, chovu, pungufu, sikivu n.k
(a) Vivumishi vya sifa
Hutaja jinsi vitu vilivyo au vinavyoonekana.
Mf; eme, pevu, nyenyekevu, nyamavu, changamfu, ovu,erevu n.k
Mf ni mtu mwema sana yule (mwerevu, mjanja,mpevu, mwovu n.k)
Sifa nyingineni Kama; zuri; eupe, eusi, gumu, baya, bovu, kubwa, rtefu, pana, nene, kongwe, imara, legevu, rahisi.
(b) Vivumishi vya idadi
Hivi hueleza idadi ya majina katika jumla ya hesabu yake. Inaweza kuwa (a) jumla (b) idadi inayojitegemea.
Vya jumla – chache, ingi, lukuki, haba, kidogo, pungufu, maridhawa, tosha, ote n.k
Vya idadi au hesabu;
-Moja, mbili, mia, ishirini, milioni, laki, elfu n.k
Mifano alipewa pesa pungufu (-------)
Hizi ni zawadi maridhawa (---------), yule mzee ana mbuzi milioni (-----------------)
(c) Vivumishi viulizi
Ni vivumishi vyenye kuuliza maswali kuhusu nomino ama kiwakilishi husika. Vivumishi hivi pia huoanishwa Kama viwakilishi viulizi tulivyovichambua.mf. –Vitu vingapi? –Kitabu kipi? –Kalamu ngapi? -Watoto wa nani? –Uzi upi? –Mwalimu nani? –Kitu gani?
(c) Vivumishi vya pekee; (enye/enyewe/ingine n.k)
hivi urejesha sifa kwa kutajwa. Hii huleta upekee kwa mf;
-Mtoto mwenyewe huyu hapa.
-Kiti chenyewe kimeshaharibika.
-Mwalimu mwingine ameletwa shuleni kwetu.
Kwa kutumia vigezo vya namna/jinsi vinavyotamkwa na mahali vinapotakiwa nini majina ya vitamkwa vifuatavyo
(a) [b]
(b) [d]
(c) [f]
Bongo chemusha ni hapa ndugu muswahili wa leo
1. Orodhesha maneno matano tu, ambayo utamkaji wake haufuati otografia ya Kiswahili.
2. Fasihi haina maana yoyote Kwa jamii zaidi ya kuchosha bongo za watunzi. Jadili kauli hii kwa mifano maridhawa.
3. Zipo nadharia kadhaa zinazoeleza chimbuko la lugha ya Kiswahili. Zitaje mbili kasha elezea moja kwa ufasaha.
4. “Nyimbo za Ninao! Ninao Subiri vipimo” eti nazo ni kazi za fasihi. Jadili.
matumizi ya neon lugha yanahusu asilia, yaani lugha asilia, yaani lugha inayotumiwa na binadamu katika mawasiliano yao kwa njia ya sauti zinazounda maneno.
Lugha asilia hutofautishwa na lugha nyingine kama vile lugha ishara, ambayo ingawa nayo hutumiwa katika mawasiliano ya binadamu lakini haitumii sauti; au lugha kompyuta, ambayo kimsingi ni lugha unde (iliyoundwa kwa makusudi maalumu) inayotumiwa na mashine. Kwa namna hiyo kila asilia tujue kwamba ina maana ya lugha ya binadamu.
Sauti za lugha asilia
Wanaisimu wengi hukubaliana kwamba lugha ya binadamu ni mfumo wa sauti nasibu zenye kubeba maana na ambazo hutumiwa na jamii Fulani ya watu kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao(massamba na wenzie,1999:1, 2001:1) sauti nasibu ni sauti ambazo uteuzi wake haukufanywa kwa kufuata mantiki au vigezo Fulani maalumu bali umetokana na makubaliano ya kimazoea tu ya watumiaji wa lugha inayohusikana hii ndiyo maana sauti za lugha mbalimbali ama zinaweza kufanana sana au kwa kiasi Fulani tu; na zinaweza pia zikasigana sana au kwa kiasi Fulani tu.
SARUFI MATAMSHI (fonolojia)
Hii ni sayansi ya lugha inayojihusisha na kanuni na jinsi ya utamkwaji wa maneno katika lugha.
Binadamu anao uwezo wa kutoa sauti zisizo ukomo lakini ni sauti chache tu huweza kuzitumia katika lugha. Sauti hizo zitumikazo hujulikana kama “VITAMKWA”. Vitamkwa vimegawanyika katika makundi makuu mawili. IRABU na KONSONANTI.
IRABU AU VOKALI AU VOKOIDI
Hivi ni vitamkwa ambavyo wakati wa utamkaji wake hewa kutoka mapafuni haipati uzuizi wowote katiaka chemba ya mdomo ama katika viungo matamshi.
SIFA
Vitamkwa hivi viko vitano tu katika kiswahili -/a/, /e/, /i/, /o/, na /u/
- tofauti baina ya kitamkwa kimoja na kingine hutegemea mwinuko au ulalo wa ulimi na umbo la mdomo.
- Sauti (vitamkwa) hizi huwa zote ni ghuna.
SIFA BAINIFU ZA IRABU
Ili kujua sifa za irabu, ni vema basi kujua kila irabu inahusisha sehemu gani ya ulimi katika kuitamka. Na ujuzi huo utakuja pale tu, tutakapojua umbo ulimi.
juu
i u
Mbele nyuma
e o
chini
a
Chini
Tunaweza kuzibainisha irabu kwa kuzingatia umbo hilo la ulimi.
Mfano /u/
- kwanza iko nyuma ya ulimi
- pili iko juu
- kasha tunatathmini umbo la mdomo tunapoitamka – mviringo.
Hivyo: /u/ {- mbele }
{+ Juu }
{+ Mviringo}
(a) kwa kuwa kuna nyuma na mbele = sifa ya nyuma ndiyo hutumika – hivyo kupata _+ nyuma
(b) kwa kuwa kuna juu na chini = sifa ya juu hutumika hivyo kupata +_ juu.
(c) Sifa ya kati huwa na sifa zote mbili ± juu.
(d) Sifa ya kati katika mbele huwa na ± nyuma.
(e) Kwa kuwa irabu si konsonanti basi sifa nyingine ni ile ya – kons.
(f) Kasha sifa ya umbo la mdomo huwa ± viringo.
Kwa maneno mengine tunaweza kuibainisha sauti moja kwa kutumia vipengele vitano kama ilivyo katika <<>>.
+ ghuna + ghuna
- kons - kons
U ni + nyuma /A/ ni
+ juu
+ viringo
U ni
TABIA ZA LUGHA
Tofauti na sifa, tabia ni mambo ambayo hujitokeza katika lugha lakini ambayo si ya lazima na mara nyingi hujitokeza kwa viwango tofauti katika lugha tofauti.
i. lugha huathiriwa na lugha zinazopakana nazo ama hata yenyewe kuathiri lugha hizo kimsamiati,kimuundo na hata kimatamshi.
ii. Lugha hukua na kuenea.
iii. Lugha huwa na lahaja zake
iv. Lugha huandikika, inaaminika kuwa kila lugha yaweza kuandikwa ama kuwekwa katika mfumo wa maandishi. Zipo lugha nyingi ambazo hazijaandikwa bado lakini hiyo haina maana kuwa haziandikiki.
v. Lugha huweza kufa na kupotea kabisa iwapo itakosa watumiaji kwa sababu zozote zile, kama majanga ya mafuriko, vita, magonjwa na ama kuhama na kutawanywa kwa watumiaji wake.
Share This :
comment 0 Comment
more_vert