MISINGI YA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI.
Uhakiki ni uchunguzi au uchambuzi wa kina wa kazi za fasihi. Uhakiki wa kazi yoyote ya fasihi unazingatia
maeneo makuu mawili. Na Kazi za fasihi huhakikiwa kwa kutumia vigezo vikuu viwili maeneo hayo ni :
· MAUDHUI.
· FANI.
MAUDHUI.
Ni yale mambo yote ambayo yamemsukuma mwandishi /msanii kuandika kazi yake.Na pia Maudhui ni mambo
anayoyasema msanii kwa walengwa au hadhira yake. Katika kipengele cha maudhui mhakiki hana budi
kuchambua mambo yafuatayo:
1. DHAMIRA
2. MIGOGORO.
3. UJUMBE.
4. FALSAFA.
5. MTAZAMO.
6. MSIMAMO.
DHAMIRA.
Ni suala linaloongelewa au kujadiliwa na mwandishi au msanii katika kazi ya sanaa. Ni kiini cha habari nzima
iliyoandikwa au kusimuliwa.Ni wazo kuu au mawazo yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Kwa mfano Ukombozi
wa mwanamke,Rushwa na Umuhimu wa elimu
MIGOGORO.
Ni mivutano au mikinzamo inayojitokeza kutokana na misuguano ya kiuchumi,kisiasa kijamii na kiutamaduni . Ni
hali ya kutoelewana baina ya pande mbili. Migogoro yaweza kuwa baina ya pande mbili au mtu binafsi. Kuna
aina mbalimbali za migogoro. Aina hizo ni pamoja na :
Kisiasa, kiuchumi,kijamii na kinafsi.
UJUMBE.
Ni mafunzo au maadili yanayopatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi ili kuweza kupata ujumbe. Ujumbe
unaweza kutamka wazi au kwa kicho. Mhakiki hana budi kujiuliza maswali yafuatayo: mwandishi anatoa
ujumbe gani kwa jamii?,anashauri nini?,je ujumbe huo unamhusu nani katika jamii?
FALSAFA.
Ni mwelekeo wa imani ya msanii ,mwandishi au msanii anaamini nini Mfano unaweza kubaini imani ya
mwandishi Fulani kuhusu mwanamke au suala zima la maisha. Na pia unaweza kuijua vizuri falsafa ya
mwaandishi kwa kusoma kazi zaidi ya moja za mwandishi anayehusika.

wa mwanamke,Rushwa na Umuhimu wa elimu.

MTAZAMO.
Ni namna mwandishi anavyoona mambo , hapa mhakiki hana budi kubaini uyakinifu wa msanii. Mhakiki ajiulize
je msanii ameandika mambo kwa kubuni au kudhani au kiuyakinifu au ameichunguza jamii kwa undani. Kwa
mfano mtazamo wa kidini unaweza kumwongoza kuona kuwa, kila jambo nimapenzi ya mungu.
MSIMAMO.
Ni uamuzi wa kufuata jambo Fulani bila kujali kukubalika au kutokukubalika kwa jambo hilo na jamii. Au ni
maoni yake juu ya mambo mbalimbali anayoyaeleza kwenye kazi yake.
comment 0 Comment
more_vert