MASIGNCLEAN101

faida za umilisi,Dhana ya utendaji, Mambo ya kuzingatia katika utumizi wa lugha,umbo la ndani na umbo la nje la sentensiDhana ya sarufi zalishi,maana ya sarufi

faida za umilisi,Dhana ya utendaji, Mambo ya kuzingatia katika utumizi wa lugha,umbo la ndani na umbo la nje la sentensiDhana ya sarufi zalishi,maana ya sarufi
citylab
Saturday 17 September 2022

 Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya kwanza ni utangulizi ambao unahusisha fasili za sarufi na sarufi zalishi, sehemu ya pili kiini cha swali na sehemu ya tatu ni hitimisho.

Dhana ya sarufi  imefasiliwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo:
Sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria na kanuni za matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake (Pei na Gaynor, 1969:88)
Sarufi ni taaluma ya lugha inayohusu uchunguzi na uchanganuzi wa kanuni na vipengele mbalimbali vya lugha (Massamba na wenzake, 2004).
Sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni na matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake(Kihore 2012).
Sarufi ni kanuni na sheria au taratibu za uchambuzi zinazotawala lugha(Massamba na wenzake, 2001).
Sarufi ni utaratibu wa kanuni ambazo humwezesha mtumiaji wa lugha kutunga tungo sahihi zinazoeleweka mara zinapotamkwa (Kapinga, 1983).
TUKI, (1999) Sarufi ni sayansi ya lugha.
Kutokana na fasili za wataalam hapo juu sarufi ni taratibu na kanuni zinazotumika katika kuunda lugha kwa kuzingatia ukubalifu wa watumiaji wake huku ikizingatia viwango vyote vya uchambuzi yaani kiwango cha maana,matamshi, miundo, na maumbo katika lugha husika.
Sarufi zalishi ilizuka kutokana na kasoro za sarufi mapokeo na sarufi miundo katika uchanganuzi wa lugha. Mtazamo huu uliasisiwa na Noam Chomsky katika kitabu chake cha syntactic structurecha mwaka (1957). Mtazamo wa sarufi zalishiulijikita katika uundji wa nadharia ambayo ingeeleza namna lugha hutumiwa na watumiaji wake hususani, jinsi wanavyotumia kanuni chache katikalugha yao kuzalisha sentensi nyingi na zisizo na kikomo. Kutokana na uwezo huu mzawa wa lugha huweza kuunda tungo ambazo ni sahihi na ambazo si sahihi (Matinde,2012).

Chomsky, amewasilisha mtazamo wa Sintaksia unaotambuliwa kama Sarufi  zalishikatika kaziyake.Chomsky alikusudia kukuza fafanuzi mwafaka za hali ya sintaksia ya lugha mbalimbali,yaani jinsi lugha mahususi zinavyounganisha maneno kuunda sentensi.Vile vile kazi hiyo ilidhamiria kukuza nadharia ya kijumla ya sintaksia inayobainisha ni mambo yapi ya kijumla yanayopatikana katika lugha mbali mbali na jinsi gani masualahayo yanavyotofautiana katika uwanja huu wa sintaksia.
“In linguistics, generative grammar is a grammar (or set of rules) that indicate the structure and interpretation of sentences which native speakers of a languages accept as belonging to the language”
Sarufi zalishi ni sarufi mkusanyiko wa kanuni inayoonesha muundo na tafsiri ya sentensi ambayo mzungumzaji wa lugha (mzawa) au mmilisi wanavyo ipokea kama ilivyo.
Dhana za msingi za nadharia za sarufi zalishi;
Umilisi, ni ujuzi au uelewa wa kanuni zinazotawala lugha fulani ambazo kila mzungumzaji wa lugha asilia huwa nao. Ujuzi huu huhodhiwa ubongoni mwa mzawa wa lughana ndio humwezesha kutunga tungo nyingi na zenye urefu wowote.
Ujuzi huu huhusu kanuni zinazotawala lugha hiyo husika. Ujuzi huu humwezesha kutambua sentensi sahihi, zisizo sahihi na kupambanua sentensi zenye utata. Pia humwezesha kupuuza makosa katika mazungumzo kama vile kuteleza kwa ulimi, na kukatisha sentensi.
Chomsky anaeleza kuwa  mtu anapojifunza lugha huanzia na umilisi na anaendelea kudai kuwa kwa kiasi kikubwa umilisi wanaokuwa nao wazawa wa lugha moja hufanana na hii ndiyo inayowafanya waelewane katika mazungumzo yao kwamba mzungumzaji anasema kile anachotaka kusema na msikilizaji anaelewa kile kilichosemwa na msikilizaji.(Rubanza,2003).
Umilisi humwezesha mzawa wa lugha;
Ø  kutambua sentensi sahihi na ambazo si sahihi mfano:
i)        (Sahihi) Mwalimu anafundisha wanafunzi darasani.
(Si sahihi)Wanafunzi anafundisha mwalimu darasni.
ii)      (Sahihi) Mtoto mdogo anaimba.
(si sahihi) Anaimba mdogo mtoto.


Ø  Kutunga sentensi nyingi zenye urefu wowote :
i)                    Msichana mrembo mrefu mweusi alikamatwa bustanini jana jioni, akiiba matunda ya mzee Juma na kupelekwa kituo kidogo cha polisi kwa maelezo zaidi.
ii)                  Mtoto mdogo aliyeanguka jana jioni na kuvunjika mkono, amepelekwa hospitalilakini bado hali yake ni mbaya hivyo madaktari wameamua kumpeleka hosipitali ya mifupa kwa uchunguzi zaidi ili kupata suluhisho la tatizo lake.
Ø  kutambua sentensi zenye maana sawa.
Mfano;
i)                    Watoto wanakula chakula.
 Chakula kinaliwa na watoto.
ii)                  Mama anapika chakula.
    Chakula kinapikwa na mama.
Ø  kutambua sentensi zenye utata, mfano;
i)                    Juma amenunua mbuzi.
Utata upo katika neno mbuzi lenye maana zaidi ya moja.
Mbuzi kama kifaa cha kukunia nazi
Mbuzi kama mnyama.
ii)                  Mama ana paa.
Utata upo katika neno paa lenye maana zaidi ya moja.
Paa kama kitendo cha kukwea juu ya, mfano mti, mlima, angani.
Paa kama mnyama aishie polini.
Ø  Kutambua muundo wa tungo katika lugha yake na vipashio vyake.
Mfano;
i)                    Mbunnge wetu amewasili jimboni.(Tungo sahili)
ii)                  Kitabu kilichopotea kimepatikana. (Tungo changamano).

Ø  Kutambua aina mbalimbali za sentensi katika lugha yake
Mfano;
i)                    Mwalimu anafundisha Kiswahili. (Sentensi arifu).
ii)                  Shika chini. (Sentensi amrishi).
iii)                Wanafunzi wangapi wamefika? (Sentensi ulizi).
iv)                Mapunda, na wewe umefika! (Senteansi mshangao).
v)                  Lugano angalikuja mapema angalimkuta Amiri. (Sentensi shurutia).

Ø  Kutambua sentensi zenye maana na zile zisizo na maana.
Mfano;
i)                    Baba analima shamba.
ii)                  Shamba analima baba.
Hivyo ili kutambua sentensi zenye maana na zile zisizo na maana, kulingana na muundo wa sentensi za kiswahili, muundo wa sentensi zilizopo katika mfano wa pili si sahihi kwani zimekiuka sintaksia ya lugha yaKiswahili.
 Utendaji ni dhana mojawapo ya sarufi zalishi, hurejelea usemaji na utumizi wa ujuzi wa mzawa wa lugha katika kutumia lugha yake ndani ya muktadha wa lugha mahususi. Utumizi huu wa lugha huzingatia :-
·         Muktadha:
Mifano,
  - Kaniletee chaki ofisini (shuleni)
-   Nani wa kuondoka? (stendi).
 - Amependeza hajapendeza? Bibi kampata bwana na bwana kampata bibi ( ukumbini).

·         Uhusiano baina ya wahusika,
Mifano;
Mchungaji na waumini;
Mchungaji: Bwana Yesu asifiwe.
Waumini: ameeeen.
Mchungaji: leo bwana amenionesha
Waumini: ameeeeeni.

Mzazi na mtoto
Mzazi:  Amina leo mmejifunza nini shuleni?
Mtoto: Tumejifuna kiswahili mama.
                         Mzazi: Vizuri mwanangu, sasa kabadilishe nguo chakula kiko jikoni,
alafu uoshe vyombo.
                       Mtoto: Sawa mama.
   Hakimu na mshtakiwa.
                        Hakimu:          Mshtakiwa una lolote la kujitetea?
                        Mshtakiwa:     Ndio mweshimiwa hakimu.
                        Hakimu:          Jitetee.
                        Mstakiwa:       Mheshimiwa  naomba mahakama inipunguzie adhabu kwa
sababu nikosa langu la kwanza pia nina familia
inayonitegemea.
 Daktari na mgonjwa.
                        Daktari:           Meza mbili kutwa mara tatu (2×3×7)
                        Mgonjwa:        Sawa daktari.
                        Daktari:           Hakikisha unakunywa maji ya kutosha.
                        Mgonjwa:        Sawa daktari.
Hivyo basi katika utumizi wa lugha uhusiano baina ya wahusika huwawezesha kuteua aina ya mazungumzo yanayostahili kulingana na mazungumzo husika.
Mada ya mazungumzo
Mfano;
Mada ya kisiasa.
Kiongozi:        “People’s”
                        Wananchi:       “Power”
Kiongozi:        Leo ni siku pekee ya kuzungumza na wananchi, naomba
mniskilize kwa  makini.
Mada ya afya.
Bwana afya:                Ndugu zangu chimbeni mashimo ili tuondokane na magonjwa ya
kuambukiza kama yanayojitokeza katika kijiji chajirani.
Wanakijiji:                   Sawa mkuu, tutatekeleza.
 Dhumuni la mazungumzo.
 Mfano;
Dhumuni la kuelimisha;
    Mshauri nasaha:      Kutokana na majibu ya vipimo vyako, inabidi ule vizuri chakula bora
ikiwa ni pamoja na matunda,pia upate muda wa kupumzika.
                                  Ukizingatiahaya utaishi kwamatumaini.
     Mgonjwa:               Sawa.
Dhumuni la kuonya.
Mazungumzo kati ya mzazi na mtoto:
Mzazi:             Siku hizi umekua ukichelewa kurudi nyumbani,  kinachokuchelewesha
                         nini?
 Mtoto:            Usafiri mama.
Mzazi:             Usafiri gani huo mpaka saa nne za usiku?  mbona Aisha amewahi
                         kurudi?
Mtoto:             (kimya).

Mtoto:             (kimya).
Mzazi:             Mwanangu dunia haiko hivyo unavyodhani, umebadilika sana siku hizi. Ujana
                      una mambo mengi, ni vyema uutumie ujana wako vizuri,  kumbuka kuna
magonjwa hatari  na yasiyotibika.
Dhumuni la kuburudisha: 
Mfano;
Mshereheshaji na wageni waalikwa:
Mshereheshaji:            Piga vigelegele kwa maharusi wetu jamani.
Wageni waalikwa:       Kilililiiiiiiiiiiiii ………………..
Mshereheshaji:            Mwenye wivuuuuu…………...
Wageni waalikwa:       Ajinyongeeeee ……………….
·         Jinsi.
Tofauti za kimaumbile baina ya ke na me hupelekea wazungumzaji wazawa wa lugha kuteua aina fulani ya lugha ya mazungumzo kutokana na jinsi zao.
Mfano;
Mazungumzo kati ya mwanamke na mwanamke:
Asha:   Mambo shosti?
Getrude:          Safi tu shoga angu.
Asha:   Nakuona umepodoka si mchezo?
Getrude:          Mambo ya mfikemo hayooo ………..
Mazungumzo kati ya mwanaume na mwanaume,
Juma:   Nambie kamanda.
   
 Hamisi:           Poa jembe langu.
  Juma:             Ishu zinaendaje?
  Hamisi:          Burudani, kuchakarika tu.
Hata hivyo utendaji huweza kuathiriwa na kasoro za kimatamshi, hasira, furaha, uchovu,ulevi na matatizo ya kumbukumbu.
Umbo la ndani.
Katika umbo hili hujitokeza katika sentensi kabla haijafanyiwa mchakato wa kimofofonolojia. Umbo la ndani hubeba maana kamili ya tungo na vipashio vya tungo hubainika bayana, kwani huwa havijafanyiwa michakato yoyote.
 Sentensi zifuatazo zina umbo la ndani:
     Kitabu alikionipa.
     Mjengi wa nyumba.
     Mpiki wa chakula.
Baada ya sentensi hizi kuambikwa viambishi vipatanishi vya kisarufi(baada ya mchakato wa kimofofonolojia)  tunapata sentensi ambazo zipo kweny umbo la nje.
     Kitabu alichonipa.
     Mjenzi wa nyumba.
     Mpishi wa chakula.
Umbo la nje;
Umbo hili hutokea baada ya umbo la ndani kufanyiwa mageuzi au mchakato wa kimofofonolojia muhimu hadi kufikia kiwango cha usemaji sahihi na unaokubalika, kwa hivyo umbo la nje hudhihirika kimatamshi na kiothografia. Umbo hili haliwezi kufanyiwa michakato zaidi.


Mifano,
               Umbo la ndani                                                    Umbo la nje
             Juma umwa maino.    Juma anaumwa meno
             Mama piki kiakula.                                              Mama anapika chakula
             Kijana mwibi.                                                       Kijana mwizi.
Uchamko;
Uchamko ni utaratibu wa kutumia sheria fulani ambazo huweza kutumika mara kwa mara katika kuunda sentensi ambazo zina urefu usio na kikomo.Uchamko, hutokana na sentensi zaidi ya moja kupachikwa katika Sentensi ile ya kwanza ili kuunda sentensi moja isiyo na kikomo, uchamko hujitokeza katika aina kuu mbili, ambao ni utegemezi na uambatanishaji.
Utegemezi;
Uteggemezi ni aina ya uchamko ambao hutokana na matumizi ya maneno kama: kuwa, kwamba, kama, na ili. Pia hutokana na hali ya kuwepo au kutokea kwa kipashio kimoja cha kiisimu ambacho hutegemea uwepo wa kipashio kingine. Utegemezi huweza  kutokana na;
Upachikaji kwa kutumia vijalizi na urejeshi ambao hutumiwa kuunda sentensi changamano.       
Mfano,                                                        
Mbuzi aliyechinjwa jana amepikwa leo.
                                                            S
                                   KN                                        KT
                    
                         N                    Î²v                 T                 E

                                                                                                                                                                                                                                                                      
                   Mbuzi     aliyechinjwa jana    amepikwa       leo.
Uambatanishaji;
Uchamko pia huweza kudhihiriishwa na uambatanishaji wa sentensi, huu ni uchamko ambao hutokana na sentensi ambbatano.
Mfano,
                                                        S
                                    KN1                               KT1

                   N1                          T1                                            S2
                                                                               KN2                    KT2

                                                                        N2                          T2              U           S3

                                                                                                                         KN3           KT3

                                                                                                                        N3            T3

                 Mtoto                 anacheza              baba         analima       na       dada       anaimba.
Dhana ya mwisho ya sarufi zalishi  ni uchamko, uchamko ni utaratibu wa kutumia sheria fulani ambazo huweza kutumika mara kwa mara katika kuunda sentensi ambazo zina urefu usio na kikomo. Uchamko hutokana na sentensi zaidi ya moja kupachikwa katika Sentensi ile ya kwanza ili kuunda sentensi moja isiyo na kikomo. Pia hutumia kanuni chache kutunga sentensi nyingi zisizo na kikomo. Uchamko umegawanyika katika sehemu mbili yaani utegemezi na uambatanishaji.


Utegemezi
Ni uchamko ambao hutokana na hali ya kuwepo au kutokuwepo kipashio kimoja cha kiisimu ambacho kinategemea uwepo wa kipashio kingine. Utegemezi hutambulishwa na maneno kama vile; ili, kwamba, kama na kuwa. (Matinde, 2012)
 Mfano; Ambakisye alijua kuwa Ndope anafahamu kuwa shule itafunga kesho.
              Asha anajua kuwa mimi najua kuwa atafaulu mtihani.

Uambatanishaji.
Ni aina ya uchamko ambao hudhihirishwa na uambatishaji wa sentensi sahili mbili au zaidi. Kwahiyo, huu ni uchamko ambao hutokana na sentensi ambatano.
Mfano;
Shangazi anapika, mama anaandaa chakula na baba anakula.






                                    





                                        S1

                         KN                                KT

         N                                    T                                          S2

 Shangazi                         anapika                    KN                                      KT

                                                                          N                 T             N          U             S3

                                                                     mama    anaandaa    chakula      na       KN        KT

                                                                                                                                N            T

                                                                                                                           baba     anakula

Kama ilivyo kwa nadharia zingine, nadharia hii pia ina ubora na udhaifu wake.
Ubora wa nadharia hii.
·         Imeweza kuonesha umilisi alionao binadamu katika lugha yake, kuwa anaweza kuzalisha tungo au sentensi mbalimbali kwa kutumia kanuni chache zilizopo katika lugha yake.Umilisi huo humsaidia mtumiaji wa lugha kuunda sentensi hizo hata kama hajui kusoma na kuandika.
·         Pia nadharia hii inaonesha kuwa kila mzungumzaji wa lugha huzifahamu vizuri kanuni chache zilizopo katika lugha yake na kuzitumia kanuni hizi katika kuwasiliana na jamii inayomzunguka.
·         Vilevile nadharia hii ya sarufi zalishi imeweza kuonesha kuwa binadamu anao uwezo wa kufafanua kipi ni sahihi na kipi sio sahihi katika uteuzi wa maneno wakati wa uzungumzaji.
·         Nadharia hii inamchukulia binadamu kama kiumbe chenye uwezo endelevu wa kuzalisha sentensi ambayo inaweza kueleweka kwa jamii inayomzunguka.
·         Pia nadharia inatuonesha kwamba upo uhusiano mkubwa kati ya akili, kufikiri na lugha.Hususan katika dhana ya utendaji mtumiaji wa lugha anatakiwa kutumia akili anapoteua lugha ya kutumia ili kuendana na muktadha.
Udhaifu wa nadharia hii.
·         Inafafanua namna au jinsi watu wanavyozungumza lugha na sio kuwaeleza wazungumze vipi lugha hiyo itumike.
·         Haitilii mkazo mabadiliko katika lugha hata kama yapo.
·         Vipengele kama umbo la ndani na umbo la nje vinaweza kumchanganya mtu anaejifunza lugha.
Hivyo ni kweli kwamba nadharia ya sarufi zalishi imeleta mapinduzi makubwa katika taaluma ya sarufi miundo.











MAREJEO
Kapinga, (2012), Katika Dafina ya Lugha: Serengeti Education Publishers (T) Ltd, Mwanza.
Kihore Y, M. Massamba, D.P. B na Msanjila, Y. P. (2012),Sarufi Maumbo ya Kiswahili
Sanifu (SAMAKISA): TUKI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Massamba, D. P. B, Kihore, Y, M na Hokororo, J. I,(2001), Sarufi Miundo ya Kiswahili
Sanifu(SAMIKISA): TUKI: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Massamba, D. P. B, na wenzake(2004),Kamsi ya Isimu Falsafa ya Lugha: TUKI,
Dar es Salaam.
Matinde, L. (2012),Dafina ya Lugha: Serengeti Education Publishers (T) Ltd, Mwanza.
Pei na Gaynor, (2012), Katika Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA): TUKI,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
TUKI, (1999), Kamsi Sanifu ya Isimu ya Lugha: Chuo Kikuu cha Dar er Salaam.
Share This :
...